Dkt. Ntuli ashinda Ukurugenzi Mkuu wa ECSA-HC

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dkt. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Dkt. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.

Dkt. Ntuli Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo, ataongoza kwa muda wa miaka mitano.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uchaguzi Februari 12, 2025, Waziri wa Afya nchini Tanzania, Jenista Mhagama amesema kuwa nafasi hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba (7) walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.

Waziri Mhagama amesema mara baada ya usaili uliofanywa na Kamati ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa nchi wanachama, Dkt. Kapologwe alipata alama za juu zaidi na kuingia katika hatua ya mwisho pamoja na wagombea wengine wawili kutoka Kenya na Malawi.

Ameeleza kuwa majina ya wagombea hao watatu yaliwasilishwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC), ambapo Dkt. Kapologwe ameibuka mshindi.Kwa ushindi huu ni dhahiri ya kwamba Tanzania inaendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa ina Watalaam wenye sifa stahiki za kushika hatamu za Uongozi kwenye Jumuiya au Mashirika ya Kimataifa na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya wengi katika uboreshaji wa huduma za Afya.

Jumuiya ya ECSA-HC ilianzishwa mwaka 1974 na inajumuisha nchi tisa (9) ambazo ni Tanzania, Malawi, Kenya, Lesotho, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Uganda pamoja na Eswatini na inashirikiana na nchi 13 zisizo wanachama ambazo ni Botswana, Burundi, Cameroon, Eritrea, Gabon, Liberia, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Seychelles, Sudan ya Kusini, Sudan, na Somalia.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

More like this

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...