Gates Foundation yaipongeza Tanzania uboreshaji afya ya msingi na kupunguza vifo vya kina mama na watoto

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kutokana na jitihada madhubuti za kuimarisha afya ya msingi na kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Pongezi hizo zimetolewa leo Januari 31, mwaka huu na Mkurugenzi Mkuu wa Gates Foundation Barani Afrika, Dkt. Paulin Basinga alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alipata fursa ya kuona jinsi inavyotoa mchango wake kwa Serikali kuimarisha upatikanaji huduma ngazi ya afya ya msingi, hospitali za rufaa za mikoa hadi Kanda na hatimaye kupunguza rufaa za wagonjwa kufika hospitalini hapo ikiwemo kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi.

Dkt. Basinga amesema taasisi anayoiongoza imefanya kazi na Serikali ya Tanzania katika maeneo ya uboreshaji programu za kilimo, masuala ya fedha kwa ujumla wake, sekta ya afya hususani kufanya tafiti zilizoibua afua mbalimbali za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Katika hatua nyingine, Dkt. Basinga ameipongeza MNH ambayo ni hospitali ngazi ya juu ya nne nchini kutokana na huduma za ubingwa na ubingwa bobezi inazotoa kwa wananchi wa ndani, mataifa jirani, mazingira bora ya utoaji huduma na utayari wa watoa huduma kuhudumia wananchi katika hospitali hiyo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amemshukuru Dkt. Basinga kutembelea hospitali hiyo na kumhakikishia kuwa hospitali hiyo kwa nafasi yake inafanya kazi kubwa kwa niaba ya Serikali katika kuimarisha huduma nchini ikiwemo huduma ngazi ya msingi hadi ngazi ya kanda.

Prof. Janabi ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na jitihada za kuongeza idadi ya zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuimarisha huduma katika maeneo hayo na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya miaka mitano.

spot_img

Latest articles

Mwendokasi: Adha kwa abiria, gubu la madereva

Na Mwandishi Wetu Inakaribia miaka 10 tangu usafiri wa mabasi ya haraka maarufu kama Mwendokasi...

Vijana wahimizwa kuendelea kulinda amani

Na Tatu Mohamed VIJANA nchini wametakiwa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza amani iliyopo kwa kuwa wao...

Serikali ya Austria kufadhili miradi ya umeme Tanzania

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Austria kupitia Benki ya UniCredit imeahidi kuipatia fedha...

NIDA yawasajili watu wenye mahitaji maalum Temeke

Na Tatu Mohamed KATIKA kuadhimisha Siku ya Utambulisho Duniani, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)...

More like this

Mwendokasi: Adha kwa abiria, gubu la madereva

Na Mwandishi Wetu Inakaribia miaka 10 tangu usafiri wa mabasi ya haraka maarufu kama Mwendokasi...

Vijana wahimizwa kuendelea kulinda amani

Na Tatu Mohamed VIJANA nchini wametakiwa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza amani iliyopo kwa kuwa wao...

Serikali ya Austria kufadhili miradi ya umeme Tanzania

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Austria kupitia Benki ya UniCredit imeahidi kuipatia fedha...