Balozi Nchimbi awafariji Mzee Makamba na Familia ya Mwambi

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kuzungumza na Mzee Yusuf Makamba leo, tarehe 25 Oktoba 2024, jijini Dar es Salaam.

Balozi Nchimbi alifika nyumbani kwa Mzee Makamba, eneo la Wazo Hill, kumfariji kufuatia msiba wa mtoto wake, Sakida Rajab Yusuf Makamba, aliyefariki dunia tarehe 12 Oktoba 2024, mjini Morogoro.

Mzee Makamba, ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, alimshukuru Balozi Nchimbi kwa kufika kumpatia pole na alitumia fursa hiyo kumpongeza pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwa juhudi zao katika kuimarisha chama.

“Sisi tunawaona, tunawasikia, na tunawafuatilia. Endeleeni kuijenga na kuimarisha CCM. WanaCCM waendelee kufanya kazi ya kujenga na kuimarisha chama kwa bidii zote. Hakuna mwingine atakayefanya kazi hiyo bali wanaCCM wenyewe,” alisema Mzee Makamba.

Mapema kabla, Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na  Issa Gavu, Katibu wa NEC ya CCM Taifa – Oganaizesheni, alifika pia kuifariji familia ya marehemu Balozi Jaka Mwambi, aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu, kufuatia msiba wa mtoto wake, Happiness Jaka Mwambi, aliyefariki dunia Oktoba 24,2024, jijini Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...

Spika wa Bunge ateta na Dk. Mwapinga, amhakikishia ushirikiano

Na Mwandishi Wetu Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani...

More like this