Zanzibar kuanza uboreshaji Daktari la wapiga kura

Na Mwandishi Wetu

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar, unatarajiwa kufanyika kwa siku saba kuanzia  Oktoba 07 hadi 13, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk amesema uboreshaji huo wa daftari utajumuisha mikoa ya Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini, Unguja Kusini, Pemba Kaskazini na Pemba Kusini.

Jaji Mbarouk amesema uboreshaji huo ambao unafanyika kwenye mzunguko wa sita kwa mujibu wa kalenda ya Tume kwa upande wa Zanzibar utahusu kuwaandikisha watanzania wote wanaoishi Zanzibar ambao wanastahili kuandikishwa kuwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Akizungumza wakati akifungua mkutano kama huo Kisiwani Unguja, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari ameongeza kuwa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya Mwaka 2024, Tume itawaandikisha watanzania waliopo Zanzibar ambao wametimiza umri wa miaka 18 na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Amefafanua kuwa mtanzania huyo atakayeandikishwa ni lazima awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yeyote na awe anastahili kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

“Kwa lugha nyepesi ni kwamba, Tume itamwandikisha mtanzania yeyote aliyopo Zanzibar ambaye amekosa sifa za kuandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Hivyo, atakayeandikishwa kwenye Daftari la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi atapiga kura moja tu ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji Asina.

Uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ulifanyika Julai 20, 2024 mkoani Kigoma na mpaka sasa uboreshaji umeshafanyika kwenye mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Singida na sehemu ya mkoa wa Dodoma.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

More like this

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...