Polisi wakabiliana na waandamanaji mjini Nairobi

Nairobi, Kenya

Makabiliano makali yamezuka katikati ya mji Mkuu wa Kenya, Nairobi, baada ya polisi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga muswada wa fedha wa 2024.

Umati wa waandamanaji ulikuwa umekusanyika katika barabara mbalimbali kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 wakati makabiliano yalipozuka.

Polisi waliwarushia vitoa machozi waandamanaji waliokuwa wamejihami kwa maji na simu za rununu ili kueleza msimamo wao dhidi ya Muswada huo.

Umati huo ulianza kukusanyika mapema saa moja asubuhi karibu na Hifadhi ya Kitaifa ya Kenya.

Vikundi hivyo vilikuwa vikiimba kauli mbiu za pingamizi dhidi ya Muswada wa fedha huku maduka kadhaa yakisalia kufungwa katika maeneo mbalimbali ya katikati ya mji huo.

Waandalizi wa maandamano hayo, vijana ambao wanafahamika kama Gen Z wanatoa wito kwa zaidi ya watu milioni moja kujitokeza na kushiriki.

Maandamano hayo yaliyopewa jina la “Kenya Reject-Finance Bill 2024,” yamekuwa yakishika kasi na kuwavuta maelfu ya watu mitaani wiki jana kutoa upinzani wao.

Kulingana na michakato ya bunge, leo hii ni hatua ambapo wabunge hupitia Mswada kifungu kwa kifungu kinachopendekeza marekebisho katika kile kinachojulikana katika lugha ya bunge kama kamati ya bunge zima.

Muswada huo ulipita awamu ya pili wiki iliyopita baada ya wabunge 204 kuunga mkono huku 115 wakiupinga. Baada ya hapo muswada huo utasogea awamu ya tatu ambapo Bunge litaupigia kura ukiwa na marekebisho mapya.

Waandamanaji wanahoji kuwa mpango wa kukusanya kodi zinazopendekezwa za katika muswada huo zitazidisha hali ngumu ya kiuchumi kwa Wakenya wa kawaida.

Siku ya Jumatatu, serikali ilionya Wakenya wanaopanga kuandamana Jumanne dhidi ya aina yoyote ya ghasia na uharibifu wa mali.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki, mbali na kukiri kwamba kila Mkenya ana haki ya kuandamana au kulaani, alisisitiza kwamba waandamanaji hawapaswi kukiuka haki na uhuru wa wengine.

spot_img

Latest articles

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...

WARAKA WA MWANDOSYA KUMBUKUMBU YA MWAPACHU

KUMKUMBUKA MAREHEMU BALOZI JUMA VOLTER MWAPACHU Balozi Juma Volter Mwapachu (Mwenyezi Mungu Amrehemu), mwanasheria, mwanadiplomasia,...

More like this

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...