MATENGENEZO YA BOMBA MPIJI YAKAMILIKA, DAWASA YAINGIA MTAANI

Na Mwandishi Wetu

HUDUMA ya maji imeanza kurejea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa matengenezo ya kinga ya bomba kuu lenye kipenyo cha inchi 72 katika eneo la Mpiji, Kata ya Mabwepande.‎‎

Hata hivyo DAWASA inaendelea kufuatilia usambazaji wake kuhakikisha inawafikia wananchi wote wanaohudumiwa na mtandao huo.

‎‎Akizungumza wakati wa kufuatilia usambazaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Ndele Mengo, amesema huduma imeanza kuimarika na kufika katika makazi ya wananchi baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo.‎‎

Amesema timu za usambazaji maji pamoja na mafundi zimeanza kufuatilia hali ya huduma katika maeneo mbalimbali ili kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza na kuhakikisha maji yanawafikia wananchi kwa kiwango kinachotakiwa.‎‎

Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati usambazaji wa maji ukiendelea kurejea katika maeneo yao.‎‎

Kwa upande wake, Mjumbe wa Shina namba 5, Mtaa wa Mtakuja, Kata ya Kunduchi, William Mwaiswelo, ameishukuru DAWASA kwa juhudi za kukamilisha matengenezo na kurejesha huduma ya maji.‎‎

Amesema wananchi walikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kipindi cha matengenezo, lakini hali imeanza kuimarika baada ya kazi hizo kukamilika.‎‎

Naye mkazi wa Mtaa wa Meko, Kata ya Kunduchi, Mariam Salum, amesema maji yalianza kurejea tangu usiku na hali ya huduma imeendelea kuwa nzuri.‎‎

“Tunaishukuru DAWASA kwa sababu tulipata usumbufu kidogo wakati wa matengenezo waliyokuwa wametangaza, lakini kwa sasa huduma imeimarika na maji yanatoka kwa msukumo mzuri,” amesema Salum.‎‎

Matengenezo ya kinga katika bomba hilo yalifanyika kwa lengo la kuimarisha usalama wa miundombinu na kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kutokana na El Niño.‎

spot_img

Latest articles

PIC yaitaka Benki ya Kilimo kupanua uwezo wa kuwafikia wakulima

Na Mwandishi Wetu KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma...

TANESCO YAJENGA NJIA MBADALA YA UMEME KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA UMEME MBAGALA, KIGAMBONI, MKURANGA NA KIBITI

📌Ni katika kuboresha hali ya upatikanaji umeme kwenye maeneo yaliyoathirika 📌MD Twange awashukuru wateja...

UJENZI WA NJIA YA KUPELEKA UMEME KISIWANI MAFIA KUNUFAISHA WANANCHI MKURANGA

📌 Ni kupitia kupata umeme wa uhakika na ajira wakati wa utekelezaji wa mradi 📌...

TANESCO YAELEZA CHANZO HITILAFU ILIYOPELEKEA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA UMEME MBAGALA, KIGAMBONI, MKURANGA NA KIBITI

📌 Ni kufuatia hitilafu katika njia ya kusafirisha umeme ya ardhini yenye msongo wa...

More like this