UJENZI WA NJIA YA KUPELEKA UMEME KISIWANI MAFIA KUNUFAISHA WANANCHI MKURANGA

📌 Ni kupitia kupata umeme wa uhakika na ajira wakati wa utekelezaji wa mradi

📌 Wananchi wapatiwa elimu namna ambavyo mradi utachochea shuhhuli za kiuchumi

Na Mwandishi wetu

WANANCHI wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kunufaika na mradi mkubwa wa njia ya kusafirisha meme ya kilovoti 33 kupitia waya maalumu itakayopita chini ya bahari kutoka Mkuranga hadi Visiwa vya Mafia.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mradi huo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Omary Said amesema utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza utoaji wa huduma ya umeme, kuchochea shughuli za uzalishaji na maendeleo kwa Wananchi.

Ameipongeza Serikali kupitia TANESCO kwa kuendelea kupanua huduma za umeme, akieleza kuwa mradi huo utakuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi, hususan katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme.

“Tunawapongeza wenzetu wa TANESCO kwa kuendelea kutanua wigo wa huduma za umeme. Tunaamini mradi huu utaleta maendeleo kwa wananchi kuongeza shughuli za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa jamii”. Amesema Bw. Said.

Ameongeza kuwa Wilaya ya Mkulanga itaendelea kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa mafanikio na ubora wa hali ya juu na kutokuwepo kwa vikwazo ili uweze Kukamilika nakua manufaa kwa Wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Mradi huo, Mha. Joffrey Katoto amesema TANESCO inatekeleza mradi wa kupeleka umeme Zanzibar na Mafia na mradi huo kwa ujumla una thamani ya dola za Marekani milioni 283.

“Mradi huu una maeneo matatu ambayo ni njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkuranga hadi Mafia Kilovoti 33, kutoka Tanga hadi Pemba kilovoti 132 na njia ya kusafirisha umeme kutoka Ununio hadi Unguja kilovoti 220”. Amesema Mha. Katoto.

Baadhi ya Wananchi na viongozi wa Vijiji katika maeneo yatakayopitiwa na mradi, wamesema semina hiyo imewasaidia kuelewa maeneo sahihi mradi utakapopita, maeneo yatakayo athiriwa na mradi pamoja na namna ya kushughulikia changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

Semina hiyo ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo, yakilenga kujenga uelewa na ushirikiano kati ya TANESCO, viongozi wa Serikali na wananchi ili kurahisisha utekelezaji wake, pamoja na kuwajengea utayari viongozi katika maeneo hayo wa kutatua kwa haraka migogoro inayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wake.

spot_img

Latest articles

TANESCO YAELEZA CHANZO HITILAFU ILIYOPELEKEA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA UMEME MBAGALA, KIGAMBONI, MKURANGA NA KIBITI

📌 Ni kufuatia hitilafu katika njia ya kusafirisha umeme ya ardhini yenye msongo wa...

CRDB, BENKI YA MAENDELEO YA CHINA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUFADHILI MIRADI MIKUBWA

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB na Benki ya Maendeleo ya China (CDB) zimesaini makubaliano...

WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZINAZOIBUKIA

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Ndomba amewataka...

Wapiga kura 213,024 watarajia kushiriki Uchaguzi Mdogo Chamwino na Kata 11

Na Mwandishi Wetu JUMLA ya wapiga kura 213,024 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la...

More like this

TANESCO YAELEZA CHANZO HITILAFU ILIYOPELEKEA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA UMEME MBAGALA, KIGAMBONI, MKURANGA NA KIBITI

📌 Ni kufuatia hitilafu katika njia ya kusafirisha umeme ya ardhini yenye msongo wa...

CRDB, BENKI YA MAENDELEO YA CHINA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUFADHILI MIRADI MIKUBWA

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB na Benki ya Maendeleo ya China (CDB) zimesaini makubaliano...

WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZINAZOIBUKIA

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Ndomba amewataka...