AFICD YAPUNGUZA MSONGAMANO WA MALORI DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu

Matumizi ya reli kusafirisha makontena kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda kwenye vituo vya kuhifadhia mizigo nje ya bandari yanaendelea kuwa miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kupunguza msongamano wa malori ndani na nje ya bandari hiyo.

Mbali na reli ya SGR, ambayo nayo imeanza kusafirisha makontena kwenda mkoani Dodoma, hatua kama hiyo imeanza kutekelezwa na African Inland Container Depot (AFICD), iliyopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam. Kupitia mfumo huo, makontena husafirishwa kwa reli kutoka bandarini na kupokelewa katika kituo hicho, ambako baadaye huchukuliwa na malori kwa ajili ya kupelekwa kwa wateja.

Akizungumza Jumatatu, Novemba 2, 2026, wakati wa ziara iliyowashirikisha wadau wa sekta ya usafirishaji, Meneja wa AFICD, Saeed Bin Argan, amesema kwa sasa kituo hicho kinapokea makontena yasiyopungua 100 kila siku kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa kutumia treni.

“Kwa sasa tunahamisha makontena yasiyopungua 100 kwa siku kutoka bandarini kwenda AFICD kwa kutumia reli. Hii inasaidia kupunguza idadi ya malori yanayohitaji kuingia bandarini kuchukua makontena,” amesema Bin Argan.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo ina vichwa viwili vya treni vyenye uwezo wa kuvuta mabehewa 60 kwa wakati mmoja, huku ikiwa na mpango wa kuongeza vichwa vingine ili kupanua huduma hiyo.

Hata hivyo, amesema changamoto iliyopo ni kutotumika kikamilifu kwa uwezo wa miundombinu hiyo kutokana na kutokuwepo kwa kiwango cha kutosha cha mizigo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia, amesema Bandari ya Dar es Salaam imefanya maboresho katika miundombinu, vifaa na mifumo ya uendeshaji, hatua zinazolenga kuongeza ufanisi wa shughuli za upakuaji na upakiaji wa mizigo.

Wakati maboresho hayo yakiendelea, msongamano wa malori umekuwa ukizua malalamiko kwa watumiaji wa barabara. Julai 11, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, aliagiza wadau wa sekta ya bandari na usafirishaji kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto hiyo.

“Njia ya Temeke, Kigamboni na Mandela hali ni mbaya. Kila unapokwenda unakuta malori yamepaki yakisubiri kwenda bandarini au kutoka. Mjazano wa magari umeibua malalamiko makubwa, watu wanaingia kazini saa tatu, saa nne,” alisema Chalamila.

Kwa kuimarisha usafirishaji wa makontena kwa reli, AFICD, ambayo iko chini ya Lake Group, inaweza kusaidia kupunguza idadi ya malori yanayoingia bandarini na muda wa kusubiri, hivyo kupunguza shinikizo la msongamano katika barabara zinazozunguka bandari. Hata hivyo, mafanikio ya mfumo huo yatategemea upatikanaji wa mizigo ya kutosha na uratibu mzuri kati ya bandari, reli na vituo vya kuhifadhia mizigo.

spot_img

Latest articles

UCSAF YAENDELEA KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeeleza kuwa unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali...

TANZANIA YATUMIA MKUTANO MKUU WA ISA INDIA KUVUTIA UWEKEZAJI WA NISHATI JUA KUFIKIA MALENGO YA DIRA 2050

📌Hatua zinazochukuliwa na Serikali kupunguza gharama za awali za uwekezaji zaelezwa Na Mwandishi Wetu TANZANIA...

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WATAHINIWA 31 WA DARASA LA SABA

Na Tatu Mohamed BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 31 wa...

MATENGENEZO YA BOMBA KUU KUPUNGUZA MAJI KWA SIKU NNE DAR NA PWANI

Na Mwandishi Wetu ‎‎WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na...

More like this

UCSAF YAENDELEA KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeeleza kuwa unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali...

TANZANIA YATUMIA MKUTANO MKUU WA ISA INDIA KUVUTIA UWEKEZAJI WA NISHATI JUA KUFIKIA MALENGO YA DIRA 2050

📌Hatua zinazochukuliwa na Serikali kupunguza gharama za awali za uwekezaji zaelezwa Na Mwandishi Wetu TANZANIA...

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WATAHINIWA 31 WA DARASA LA SABA

Na Tatu Mohamed BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 31 wa...