WANANCHI TABORA NA KATAVI KUNUFAIKA NA UMEME WA UHAKIKA, TANESCO YAANZA UFUNGAJI WA TRANSFOMA YA MVA 150

📌 Ni sehemu ya Utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuimarisha upatikanaji wa umeme mkoani Katavi.

📌 Transfoma mpya itaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Shinyanga kwenda Tabora na Katavi ili kukidhi ongezeko la mahitaji na ubora wa umeme.

📌 Kazi ya ufungaji kukamilika ndani ya siku 21

Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa mikoa ya Tabora na Katavi wanatarajiwa kunufaika na huduma bora ya umeme baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanza kufunga transfoma mpya yenye uwezo wa MVA 150 katika Kituo cha Kupokea na kupoza Umeme cha Ibadakuli mkoani Shinyanga.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ya kuimarisha upatikanaji wa umeme, hususan katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, ili wananchi waweze kupata huduma inayokidhi mahitaji yao na kuendesha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa ufanisi.

Akizungumza Oktoba 28, 2026, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mkurugenzi wa Kanda ya Magharibi, Mhandisi Richard Swai, amesema kazi ya ufungaji ilianza Oktoba 27, 2026, na inatarajiwa kukamilika ndani ya siku 21.

Amesema kukua kwa shughuli za kiuchumi katika mikoa hiyo kumeongeza mahitaji ya umeme, hivyo transfoma hiyo mpya itaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Shinyanga kwenda Tabora na Katavi.

“Tunachokifanya kwa sasa ni kuondoa transfoma ya awali yenye uwezo wa MVA 50 na kufunga transfoma mpya yenye uwezo wa MVA 150. Hatua hii inalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme na kukidhi mahitaji yanayoongezeka katika mikoa ya Tabora na Katavi,” amesema Mhandisi Swai.

Ameeleza kuwa wakati kazi hiyo ikiendelea, kunaweza kuwa na upungufu wa upatikanaji wa umeme katika maeneo yanayohudumiwa na miundombinu hiyo, hivyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu hadi kazi itakapokamilika.

Amesema TANESCO itaendelea kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya kazi hiyo ili wananchi wafahamu hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma ya umeme.

Kwa upande wake, Meneja wa Vituo vya Kupoza Umeme, Mhandisi Joseph Mongi, amewahakikishia wananchi kuwa kazi hiyo itatekelezwa kwa haraka na kukamilika ndani ya muda uliopangwa, ili kuwawezesha kunufaika na ongezeko la uwezo wa miundombinu ya umeme.

Uamuzi huo unafuatia maelekezo ya Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuhusu umuhimu wa kuboresha upatikanaji wa umeme kwa wananchi wa Katavi, hususan wilaya ya Mpanda.

Awali, mahitaji ya umeme katika eneo la Mpanda yalikuwa kati ya megawati 53 na 60, huku kukamilika kwa kazi hiyo kukitarajiwa kuwezesha eneo hilo kupata hadi jumla ya megawati 80 za umeme.

Uboreshaji huo wa miundombinu unalenga kukidhi mahitaji ya umeme yanayoongezeka na kuweka mazingira bora kwa wananchi kufanya biashara, kuendesha shughuli za uzalishaji na kupata huduma za kijamii zinazotegemea umeme.

spot_img

Latest articles

SELF MF YATOA MIKOPO YA SH BILIONI 138

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Huduma Ndogo za Kifedha (SELF Microfinance Fund) umetoa...

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA TANESCO KATIKA HAFLA YA UTIAJI SAINI LESENI ZA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI

📌Aelezwa jinsi TANESCO inavyozalisha Umeme kupitia Vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwemo gesi asilia Na Mwandishi...

TMIC 2026 KUFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI WA MADINI TANZANIA

Nchi zaidi ya 38 na Mawaziri zaidi ya 30 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo Utafiti wa...

More like this

SELF MF YATOA MIKOPO YA SH BILIONI 138

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Huduma Ndogo za Kifedha (SELF Microfinance Fund) umetoa...

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA TANESCO KATIKA HAFLA YA UTIAJI SAINI LESENI ZA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI

📌Aelezwa jinsi TANESCO inavyozalisha Umeme kupitia Vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwemo gesi asilia Na Mwandishi...