SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini

▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta ya madini

▪️Asilimia 10 ya mapato ya makusanyo ya maduhuli ya madini kulekekezwa kwenye utafiti▪️

Waziri Mavunde awasilisha mpango wa utekelezaji wa VISION 2030

● Kamati ya Bunge yataka mpango huo usaidie wachimbaji wadogo kutokuchimba kwa kubahatisha

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Wizara ya Madini imeandika kurasa mpya katika sekta ya madini baada ya kutangaza rasmi kuanza kwa mradi mkubwa wa utafiti wa kina wa rasilimali za madini nchini.

Tofauti na miaka ya nyuma ambapo shughuli za namna hiyo zilitegemea wafadhili au mikopo ya nje, mradi huu mkubwa wa sasa utagharamiwa kwa asilimia 100 kwa kutumia fedha za ndani zilizokusanywa kutoka kwenye sekta hiyo.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 16,2026 na Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Vision 2030 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambapo Waziri Mavunde ameeleza kuwa, hatua hii inafuatia uamuzi wa kimkakati wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuridhia mabadiliko ya kisheria yanayoelekeza asilimia 10 ya mapato yasiyo ya kodi (maduhuli) yanayokusanywa na sekta ya madini kutengwa maalum na kuelekezwa kwenye shughuli za utafiti wa jiosayansi.

Mavunde, amebainisha kuwa lengo kuu la Serikali chini ya Dira ya Sekta ya Madini ya 2030 (Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri) ni kupanua wigo wa utafiti wa kina wa jiofizikia wa anga (High Resolution Airborne Geophysical Survey) ili kuepuka uchimbaji wa kubahatisha.

“Utafiti huu mkubwa utaiwezesha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kupata taarifa nyingi na sahihi za jiosayansi.Kupitia takwimu hizi, tutabaini kwa usahihi maeneo gani wapewe wawekezaji, wachimbaji wakubwa, na hususan wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakipoteza mitaji kwa kukosekana kwa data za kisayansi,” amesema Mavunde.

Akielezea mwenendo wa tafiti za madini nchini, Mavunde alieleza kuwa, hadi sasa, ni asilimia 16 tu ya eneo lote la nchi ya Tanzania ambalo limefanyiwa utafiti wa kina wa jiofizikia, huku asilimia 84 iliyobaki ikiwa bado haijafikiwa na teknolojia hiyo.

Serikali imejipanga kutumia fedha hizi za ndani kuongeza kasi ili kufikia angalau asilimia 50 ya eneo la nchi ifikapo mwaka 2030.

Hatua hii pia imeungwa mkono na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Simon Songe, ambapo Kamati imeipongeza Serikali kwa kuondoa kabisa utegemezi wa mifuko ya nje na kuamua kutenga fedha za ndani pekee kwenye bajeti ya maendeleo ya utafiti, jambo linaloipa nchi nguvu ya kulinda siri na umiliki wa data zake za kimkakati.

Songe ameongeza kuwa, kukamilika kwa utafiti huu kutawasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuweza kuchimba kwa kufuata taarifa sahihi za utafiti jambo litakalopelekea uchimbaji wa uhakika pamoja na kuongeza mapato kwa taifa kutokana na uwekezaji mkubwa utakaojitokeza,

spot_img

Latest articles

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

WAZIRI MKUU ASISITIZA AFRIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA USAFIRI WA MAJINI

Na Tatu Mohamed WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano...

NDEJEMBI: MRADI WA TAZA KUWA CHACHU YA MAENDELEO YA KIUCHUMI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

📍 Akagua maendeleo ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme TAZA Sumbawanga na Songwe 📍...

More like this

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

WAZIRI MKUU ASISITIZA AFRIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA USAFIRI WA MAJINI

Na Tatu Mohamed WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano...