DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya huduma kwa Wateja kwa kutoa misaada kwa wahitaji wenye ulemavu kupitia Shirika lao la Equal Right for All lenye makazi yake Mabibo katika Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Asasi ya Haki Sawa kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania na unajumuisha viti mwendo, baiskeli za magurudumu matatu, fimbo za kusaidia watu wenye ulemavu wa kuona, magongo ya kutembelea na mafuta maalumu kwa watu wenye ualbino.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja DAWASA, CPA (T) Ritamary Lwabulinda, amesema huduma bora kwa mteja haiishii katika upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira pekee, bali pia inahusisha kujali na kuunga mkono makundi mbalimbali katika jamii.

“Natoa wito kwa jamii kuwashika mkono watu wenye uhitaji ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali na kuchangia maendeleo ya taifa,” amesema Lwabulinda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Asasi ya Haki Sawa kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania, Said Halili, ameishukuru DAWASA kwa msaada huo na kuzitaka taasisi na wadau wengine kuiga mfano huo wa kuwajali watu wenye ulemavu.

spot_img

Latest articles

DCEA yaibuka mshindi wa kwanza Tuzo ya uandaaji Bora wa Taarifa za Hesabu 2024/25

NA MWANDISHI WETU MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi...

MIAKA 95 YA KULIANGAZIA TAIFA: TANESCO YAANDIKA HISTORIA MPYA YA NISHATI — MBOSSA

📌 Shirika lafikisha wateja milioni 6 na uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 4,600. 📌...

WAZIRI HOMERA AIPONGEZA TANESCO KWA MAFANIKIO, IKITIMIZA MIAKA 95

📌Asema imejipanga kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme na kufikia megawati 8,000 📌Aeleza Serikali inatambua mchango...

OTR na Newrest zatupia jicho masoko mapya

Na Mwandishi wa OTR Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya kimataifa ya Ufaransa ya huduma za...

More like this