MAKAMU MWENYEKITI UVCCM SOMBI ATEMBELEA KIKUNDI CHA UKOMBOZI WA VIJANA KALAMBO

Na Mwandishi Wetu

IKIWA ni sehemu ya shughuli za Wiki ya UVCCM 2026, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC), ametembelea Kikundi cha Ukombozi wa Vijana wilayani Kalambo, Rukwa, kinachojihusisha na utengenezaji wa sofa, viti, meza, vitanda na fanicha nyingine.

Kikundi hicho cha Vijana kilichonufaika na mkopo kutoka Halmashauri ya Kalambo, uliotumika kununua vifaa vya kisasa, kuboresha karakana na kuongeza mtaji wa kuendesha shughuli zao.

Sombi amewapongeza vijana hao kwa kutumia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali na kuwataka kuendelea kuzitumia kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.Ziara hiyo ni sehemu ya Wiki ya UVCCM 2026.

Kaulimbiu “Mazingira tofauti, fursa sawa kwa vijana,” inayolenga kuwakutanisha vijana, kusikiliza changamoto zao na kuhamasisha matumizi ya fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo.

spot_img

Latest articles

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...

BRELA YAFUNGUA FURSA YA URASIMISHAJI KWA WADAU WA UCHUMI WA UBUNIFU ARUSHA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI (MNEC) AZINDUA WIKI YA UVCCM 2026 KALAMBO, ASISITIZA FURSA SAWA KWA VIJANA

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi Omary (MNEC), amezindua rasmi...

RIBA YA BENKI KUU YAENDELEA KUBAKIA ASILIMIA 6.25

Na Tatu Mohamed BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kubakiza Riba ya Benki Kuu (CBR)...

More like this