BANDA LA DAWASA LAVUTIA USHIRIKI VIONGOZI NA WAGENI COP12

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) inashiriki Mkutano wa 12 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP 12) kuhusu usimamizi wa Mazingira ya Pwani ya Bahari ya Hindi, unaofanyika Jijini Dar Es Salaam ukijumuisha zaidi ya wajumbe 500 kutoka Nchi mbalimbali wanachama.

Mkutano huo, ambao umeanza Oktoba 6, 2026 unakutanisha Nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi ulio chini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) huku ukilenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya ulinzi, usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya bahari na ukanda wa Pwani katika kanda ya bahari ya Hindi ya Magharibi (WIO).

Miongozi mwa Viongozi waliopita katika banda hilo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Nanauka ambaye amepongeza ushiriki wa DAWASA katika mkutano huo muhimu na kusisitiza elimu ya mabadiliko ya Tabianchi na athari zake kwenye sekta ya Maji ipewe kipaumbele kwa Jamii.

DAWASA ikiwa Moja ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maji inaonyesha shughuli zake sambamba na lengo la Mkutano huku ikionyesha utekelezaji wa miradi ya usafi wa Mazingira ya kimkakati wa Mbezi beach na Buguruni pamoja na mradi wa Bwawa la Kidunda unaolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

spot_img

Latest articles

DCEA yaibuka mshindi wa kwanza Tuzo ya uandaaji Bora wa Taarifa za Hesabu 2024/25

NA MWANDISHI WETU MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi...

MIAKA 95 YA KULIANGAZIA TAIFA: TANESCO YAANDIKA HISTORIA MPYA YA NISHATI — MBOSSA

📌 Shirika lafikisha wateja milioni 6 na uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 4,600. 📌...

WAZIRI HOMERA AIPONGEZA TANESCO KWA MAFANIKIO, IKITIMIZA MIAKA 95

📌Asema imejipanga kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme na kufikia megawati 8,000 📌Aeleza Serikali inatambua mchango...

OTR na Newrest zatupia jicho masoko mapya

Na Mwandishi wa OTR Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya kimataifa ya Ufaransa ya huduma za...

More like this