IDARA YA UTAFITI, MIPANGO NA UWEKEZAJI TANESCO WAASWA KUFANYA KAZI KWA UBUNIFU

📌 Wapongezwa kwa mafanikio ya miradi

📌Watumishi watakiwa kuongeza kasi, teknolojia na matumizi ya wataalamu wa ndani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeitaka Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI) kuongeza kasi katika utekelezaji wa mipango na miradi ya kimkakati, likisisitiza matumizi ya teknolojia, wataalamu wa ndani na uzingatiaji wa muda na mikataba ili kuongeza ufanisi wa katika utelelezaji wa miradi.

Wito huo umetolewa Septemba 17, 2026 na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Mhandisi Jahulula Jahulula, akimuwakilisha Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Ziwa wakati akifunga Kikao Kazi cha Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI Forum), kilichofanyika kwa siku nne katika Ukumbi wa Rockcity Jijini Mwanza.

“Idara yenu ni injini ya TANESCO, kwa kuwa mipango ya miradi mikubwa ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme, utafiti na uwekezaji inaanzia katika kazi zinazofanywa na idara yenu, hivyo mafanikio yake yana nafasi kubwa katika kuipeleka TANESCO na Taifa katika hatua za juu zaidi”. Amesema Mha.Jahulula.

Aidha, Amepongeza watumishi wa idara PRI kwa mchango wao katika utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati,ikiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere(JNHPP)lenye uwezo wa megawati 2,115, Mradi wa Umeme wa jua wa Kishapu, njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma, kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa njia ya ya kusafirisha umeme ya kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi mgodi wa GGM.

Amesema kupitia PRI, TANESCO pia inaendelea na miradi ya usafirishaji wa umeme wa kikanda, ikiwemo Tanzania-Zambia Interconnector (TAZA), huku maandalizi ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Tanzania na Malawi, Msumbiji, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yakiendelea.

“Kila mmoja wetu sasa anapaswa kufahamu kuwa Shirika linamtegemea na nchi inamtegemea. Endeleeni kuchapa kazi kwa bidii, uzalendo na uadilifu,” amesema Mhandisi Jahulula.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...