Rais Samia azindua Kituo cha kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi Agosti 22, 2026, amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), kilichopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

JNHPP ni mradi mkubwa wa kimkakati katika sekta ya nishati nchini, wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 kupitia mitambo tisa, kila mmoja ukiwa na uwezo wa Megawati 235.

Mradi huo umegharimu takribani Shilingi trilioni 7.452, fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025.

Uzinduzi huo unaashiria hatua muhimu katika juhudi za Serikali za kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuongeza uzalishaji, kuchochea uwekezaji na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati, hadi Mei 31, 2026, JNHPP ilikuwa imechangia nusu ya umeme wote unaozalishwa na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Mradi huo pia unatajwa kuwa na mchango katika kuimarisha usalama wa nishati nchini na kupunguza changamoto za upungufu wa umeme zilizokuwa zikisababisha mgao katika vipindi vya nyuma.

Pamoja na kwamba kituo hicho kunatumia teknolojia ya hali ya juu, lakini habari njema ni kwamba kinaendeshwa na Watanzania kwa asilimia 100.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya...

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...

BRELA YAFUNGUA FURSA YA URASIMISHAJI KWA WADAU WA UCHUMI WA UBUNIFU ARUSHA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM SOMBI ATEMBELEA KIKUNDI CHA UKOMBOZI WA VIJANA KALAMBO

Na Mwandishi Wetu IKIWA ni sehemu ya shughuli za Wiki ya UVCCM 2026, Makamu...

More like this