MHANDISI SWEDI: NANENANE NI FURSA YA KUIMARISHA SEKTA YA MADINI

Na Mwandishi Wetu

KAIMU Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Aziza Swedi, amesema Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu la kuwaelimisha wananchi kuhusu Sekta ya Madini, kusikiliza maoni yao na kupata mrejesho unaosaidia kuboresha huduma na kuongeza thamani ya sekta hiyo.

Mhandisi Swedi amesema hayo baada ya kutembelea mabanda ya Taasisi za Wizara ya Madini katika kilele cha Maonesho ya Nanenane jijini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika maendeleo ya sekta hiyo.

Amesema maonesho hayo yanawezesha Tume ya Madini kuwafikia wananchi moja kwa moja, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kupata maoni ambayo yanaweza kutumika kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.

“Kila swali na hoja inayotolewa na mwananchi ni muhimu, kwa sababu inatusaidia kutambua maeneo yanayohitaji maboresho na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma,” amesema Mhandisi Swedi.

Aidha, amesema ushiriki wa wananchi katika Maonesho ya Nanenane unaimarisha ushirikiano kati ya Serikali, taasisi zinazohusika na Sekta ya Madini na jamii, sambamba na kuwawezesha wananchi kupata uelewa kuhusu huduma, fursa na shughuli mbalimbali zinazopatikana katika sekta hiyo.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Swedi ametembelea mabanda ya Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), ambako amepata fursa ya kujionea huduma na shughuli zinazotekelezwa na taasisi hizo.

Amewahimiza wananchi kutumia kikamilifu fursa inayotolewa na Maonesho ya Nanenane kwa kujifunza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu Sekta ya Madini.

Pia, amewakaribisha wananchi kufika katika ofisi za Tume ya Madini na taasisi nyingine zinazohusika na sekta hiyo ili kupata ufafanuzi na huduma zaidi kuhusu masuala ya madini.

spot_img

Latest articles

SOKO BUBU LA MADINI LAGUNDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

▪️Watuhumiwa 14 wakamatwa na tuhuma za utoroshaji madini ▪️Waigeuza nyumba ya kupanga kama soko ▪️Waziri Mavunde...

Msajili wa Hazina ateta na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais...

Zimamoto yatoa elimu ya uokoaji, yakazia hatua za awali wakati wa majanga

Na Mwandishi Wetu, Dodoma JESHI la Zimamoto na Uokoaji limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu...

Mfumo wa T-CAMS ni Mageuzi ya Kidijitali Yanayojenga Uwazi, Ufanisi na Ushindani katika Sekta ya Uwakala wa Forodha Tanzania

Na Mwandishi Wetu KATIKA dunia ya sasa, ushindani wa biashara haupimwi tena kwa ukubwa...

More like this