UKAGUZI WA MIGODI WAIMARISHA USALAMA, UHIFADHI WA MAZINGIRA

Tume ya Madini yasisitiza uchimbaji unaozingatia sheria, afya na maendeleo endelevu

Na Mwandishi Wetu

TUME ya Madini imeendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi nchini ili kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia sheria, usalama wa wafanyakazi, afya kazini na utunzaji wa mazingira, hatua inayolenga kujenga sekta ya madini yenye tija na endelevu.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Mjiolojia na Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini, Paschal Juma, amesema Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira chini ya Mkurugenzi wake, Mhandisi Hamisi Kamando, ina jukumu la kusimamia na kufuatilia shughuli zote za uchimbaji ili kuhakikisha zinazingatia Sheria ya Madini, kanuni, sera na miongozo mbalimbali ya sekta hiyo.

Amesema Kurugenzi hiyo hufanya ukaguzi wa usalama na afya mahali pa kazi, hufuatilia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira, urejeshaji wa maeneo yaliyochimbwa pamoja na mipango ya ufungaji migodi kwa kuzingatia viwango vinavyolinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, amesema Kurugenzi hiyo hupitia na kuidhinisha mipango ya uchimbaji, taarifa za utendaji wa migodi na usanifu wa miundombinu ya migodi, huku ikisimamia matumizi salama ya baruti kwa mujibu wa Sheria ya Baruti, Sura ya 45, na kanuni zake.

Paschal amesema Tume ya Madini inatumia Maonesho ya Nanenane kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi, wachimbaji na wadau wa sekta kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga, mbinu salama za uchimbaji, utunzaji wa mazingira pamoja na uhifadhi na matumizi salama ya baruti.

Amesisitiza kuwa elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wadau, kuimarisha uzingatiaji wa sheria na viwango vya usalama, kupunguza ajali migodini na kuendeleza sekta ya madini inayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa kwa njia endelevu.

spot_img

Latest articles

Mlugu Mtanzania wa kwanza kutinga robo fainali mashindano ya Judo Jumuiya ya Madola 2026

Glasgow, Scotland Mchezaji wa Judu, Andrew Mlugu, ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kutinga...

FURSA ZA BIASHARA ZA MABILIONI KATIKA MIGODI ZAWAFUNGUKIA WATANZANIA

Vijana na wanawake wapewa kipaumbele kunufaika na mnyororo wa thamani wa madini Na Mwandishi Wetu...

GST yaongeza kasi ya tafiti za kijiosayansi kuvutia uwekezaji sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeongeza kasi ya...

UDSM wabuni mfumo wa simu janja unaosaidia wakulima kutumia maji kwa ufanisi

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimebuni mfumo wa kidijitali unaotumia...

More like this