Wahoo yang’ara Champion Rise Swimming Development Gala

Na Winfrida Mtoi

Klabu ya mchezo wa kuogelea ya Wahoo imeibuka kinara wa mashindano ya kuibua na kuendeleza vipaji mchezo huo ‘ Champion Rise Development Swimming Gala’ yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 10-11, 2026 katika bwawa la kuogelea la Shabaan Robert, jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo iliyoshirikisha waogeleaji chipukizi zaidi 180, yameandaliwa Champion Rise Sport kwa ushirikiano wa World Aquatics, Africa Aguatics na Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA).

Timu ya Wahoo Swim Club, imekuwa mshindi wa kwanza baada ya kujikusanyia pointi 1,648, nafasi ya pili imechukuliwa na Monti Aqua Force iliyopata pointi 1,388, namba tatu ni Malaika Aqua Eagles ikiwa na pointi 1362.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Maguzu amesema vipaji vimeonekana , kilichobaki ni kuviendeleza huku akiwaomba wazazi kuwatafutia makocha wakuwafundisha wale watoto ambao hawapo katika vilabu.

Naye Mwenyekiti wa TSA, Eng. David Mwasyoge  ameeleza kuwa mashindano ya aina hiyo yanaongeza wigo wa kupata wachezaji bora wakuiwakilisha nchi katika michuano mbalimbali ya kimataifa.

Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo,Amina Mfaume amejivunia uwepo wa vipaji vingi na kuahidi kuwa watahakikisha vinaendelezwa na havipotei.

spot_img

Latest articles

HESLB: SH800 BILIONI ZA MIKOPO BADO HAZIJAREJESHWA

Na Tatu Mohamed BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wanufaika...

SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- MHE LONDO

📌SERIKALI ITAENDEA KUHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI- MHE LONDOAfungua kikao cha Baraza...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI ASHIRIKI KONGAMANO LA WIKI YA VIJANA KITAIFA 2026

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi Omary (MNEC), ameshiriki Kongamano...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI (MNEC) APOKELEWA NKASI, AHIMIZA VIJANA KUUNGANISHA SIASA NA UCHUMI

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi Omary (MNEC), amepokelewa kwa...

More like this