TRANSFOMA NNE ZASAFIRISHWA KWENDA MRADI WA TAZA

📌 Utekelezaji wa agizo la MD Twange la kukamilisha TAZA ifikapo Novemba 15, 2026

📌 Transfoma mbili ziko njiani kutoka Dar es Salaam, nyingine mbili zimefika Iringa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TIMU mbili za usafirishaji wa transfoma nne kubwa zimeanza safari kutoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea kwenye vituo vya kupoza umeme vya Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 wa Iringa–Kisada–Mbeya–Tunduma–Sumbawanga katika Mradi wa TAZA, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange.

Timu ya kwanza inaelekea Kituo cha Iganjo mkoani Mbeya na Kituo cha Mkangamo mkoani Songwe, huku timu ya pili ikiwa na transfoma mbili ambazo tayari zimefika mkoani Iringa.

Meneja wa Mradi wa TAZA, Mhandisi Kelvin Mwasege, amesema usafirishaji huo unalenga kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kuanza kuchaji njia ya umeme kutoka Kituo cha Tagamenda Iringa kuelekea Sumbawanga kabla ya Novemba 15, 2026.

“Zoezi hili ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, kuhakikisha kabla ya tarehe 15 Novemba 2026 tunachaji njia yetu ya umeme inayoanzia Kituo cha Tagamenda Iringa kuelekea Sumbawanga,” amesema Mhandisi Mwasege.

Mhandisi wa Mradi wa TAZA anayesindikiza transfoma hizo karika timu ya pili, Mhandisi Esau Magori, amesema transfoma yenye uwezo wa MVA 250 itawekwa katika Kituo cha Kupoza Umeme cha Iringa, huku yenye MVA 200 ikiwekwa katika Kituo cha Kisada.

“Hapa tuna transfoma mbili, ambapo yenye MVA 250 tutaifunga kwenye Kituo cha Kupoza Umeme cha Iringa na ya MVA 200 tutaifunga Kituo cha Kupoza Umeme cha Kisada,” amesema Mhandisi Magori.

Amesema kukamilika kwa Mradi wa TAZA kutaiunganisha Rukwa kwenye Gridi ya Taifa na kuweka mazingira ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Tanzania na Zambia kwa ajili ya biashara ya umeme.

“Umuhimu wa huu mradi utasaidia kuunganisha Mkoa wa Rukwa kwenye Gridi ya Taifa na zaidi ya yote utakwenda kuiunganisha Tanzania na Zambia katika biashara ya kuuziana umeme,” amesema Mhandisi Magori.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, alitoa agizo la kukamilisha mradi huo ifikapo Novemba 15, 2026, alipokutana na wakandarasi na wasimamizi wa Mradi wa TAZA mkoani Iringa.

spot_img

Latest articles

RIBA YA BENKI KUU YAENDELEA KUBAKIA ASILIMIA 6.25

Na Tatu Mohamed BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kubakiza Riba ya Benki Kuu (CBR)...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM, SOMBI KUZINDUA WIKI YA VIJANA WA CCM

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) atazindua Wiki...

BANDA LA DAWASA LAVUTIA USHIRIKI VIONGOZI NA WAGENI COP12

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA)...

KABUDI: VYAMA VYA SIASA VIENDELEE KUJENGA UTAMADUNI WA MAZUNGUMZO

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu,...

More like this

RIBA YA BENKI KUU YAENDELEA KUBAKIA ASILIMIA 6.25

Na Tatu Mohamed BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeendelea kubakiza Riba ya Benki Kuu (CBR)...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM, SOMBI KUZINDUA WIKI YA VIJANA WA CCM

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) atazindua Wiki...

BANDA LA DAWASA LAVUTIA USHIRIKI VIONGOZI NA WAGENI COP12

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA)...