Akwilapo: Teknolojia mpya muhimu kukabiliana na mahitaji ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, ametoa wito kwa wadau wa sekta ya ujenzi kutumia teknolojia mpya na mbinu bunifu ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya nyumba na miundombinu nchini.

Akwilapo ameyasema hayo leo, Septemba 23, 2026 wakati akifungua rasmi maonesho ya kimataifa ya ujenzi na vifaa vya ujenzi, Builders Expo, jijini Dar es Salaam, akisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia za kisasa katika kuendeleza sekta hiyo.

Amesema kasi ya ukuaji wa miji na ongezeko la watu linahitaji matumizi ya teknolojia zitakazowezesha ujenzi wa nyumba na miundombinu kwa ufanisi, ubora na kuzingatia mahitaji ya maendeleo endelevu ya mijini.

Waziri huyo amesema sekta ya ujenzi ina nafasi kubwa katika maendeleo ya Tanzania, hivyo Serikali, sekta binafsi, wataalamu, wakandarasi na wazalishaji wa vifaa wanapaswa kushirikiana katika kutafuta na kutumia teknolojia zinazokidhi mahitaji ya sasa na yajayo.

Akwilapo amewataka wadau kujiuliza teknolojia gani itatumika katika ujenzi wa siku zijazo, akisisitiza kuwa suala si kama Tanzania itajenga, bali ni teknolojia gani itatumika katika kujenga. “Swali muhimu lililo mbele yetu leo si kama tutajenga, bali ni teknolojia za aina gani za ujenzi zitahitajika katika nyakati hizi,” alisema.

Amesema Builders Expo ni fursa kwa wadau kujifunza teknolojia mpya, kubadilishana ujuzi, kupata vifaa vya kisasa na kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji utakaosaidia kuongeza ufanisi katika sekta ya ujenzi.

Maonesho hayo yanayofanyika kuanzia Septemba 23 hadi 25, 2026, yamewakutanisha wazalishaji, wakandarasi, wataalamu, wawekezaji na wasambazaji wa teknolojia na vifaa vya ujenzi kutoka Tanzania na nje ya nchi.

spot_img

Latest articles

MKOA WA RUKWA MBIONI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Iringa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya...

FILAMU YA ‘THE RHINO OF NGORONGORO’ YAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro KATIKA kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, inayoadhimishwa Septemba 22 kila mwaka,...

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

More like this