WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026

Na Mwandishi Wetu

MAAFISA wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano na teknolojia za kidijitali zinazotolewa na TTCL.

Katika banda hilo, wananchi wanapata fursa ya kujionea huduma za intaneti ya kasi ya juu, suluhisho za kidijitali kwa matumizi ya nyumbani na biashara, pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL.

Sambamba na hilo, TTCL inaendelea kuwapatia wateja ofa maalum za Sabasaba, zikiwemo vifaa vya mawasiliano vinavyopatikana kwa bei zenye punguzo kubwa, pamoja na huduma mbalimbali zinazolenga kurahisisha maisha na shughuli za kila siku katika mazingira ya kidijitali.

Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Banda Bi. Janeth Maeda amesema ushiriki wa Shirika katika Sabasaba 2026 unalenga kuwasogezea wananchi huduma, kuongeza uelewa kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na TTCL, pamoja na kujenga mahusiano imara na wateja na wadau mbalimbali.

Aidha, alibainisha kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa Shirika kupokea mrejesho wa wateja ili kuendelea kuboresha huduma na kuendana na mahitaji ya soko la mawasiliano linalobadilika kwa kasi.

Aidha,wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kutumia buree public Wi-Fi inayopatikana katika viwanja hivyo ili kufahamu speed ya intanet ya TTCL.

TTCL inaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Shirika hilo katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere ili kujionea teknolojia bunifu, kupata elimu kuhusu huduma za mawasiliano na kunufaika na ofa maalum zinazopatikana katika kipindi chote cha maonesho.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this