Profesa Kabudi: Serikali yaendelea kuboresha huduma kwa wananchi kupitia Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, wanasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zao kwa wakati.

Profesa Kabudi alitoa kauli hiyo alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba. Aliwahimiza wananchi kutumia fursa ya maonesho hayo kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Alieleza kuwa banda la Ofisi ya Waziri Mkuu limeandaliwa kama kituo cha huduma jumuishi kinachowawezesha wananchi kupata taarifa, ushauri na msaada kutoka taasisi mbalimbali za Serikali katika eneo moja.

“Maonesho haya ni fursa kwa wananchi kufahamu majukumu ya Serikali, kupata elimu na kuwasilisha changamoto zao ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati,” alisema Profesa Kabudi.

Alifafanua kuwa banda hilo linajumuisha Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu inayosimamia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, hali inayorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Kwa mujibu wake, wataalamu waliopo bandarini humo wanatoa ushauri wa kitaalamu, kupokea kero za wananchi na kuwaelekeza hatua stahiki za kuzitatua kulingana na mamlaka ya kila taasisi.

Akizungumzia huduma zinazotolewa, Profesa Kabudi alisema vijana waliomaliza kidato cha nne wanapatiwa ushauri kuhusu uchaguzi wa tahasusi za kidato cha tano ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kielimu na kujiandaa kwa fursa za ajira za baadaye.

Aidha, wananchi wanapata elimu kuhusu masuala ya kazi, ajira na hifadhi ya jamii, ikiwemo usajili wa wanachama, mafao pamoja na huduma zinazotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Profesa Kabudi aliongeza kuwa Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu yana umuhimu wa kipekee kwani yanafanyika wakati Serikali ikiendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kuona mafanikio yaliyofikiwa na mwelekeo wa maendeleo ya nchi.

Aliwahimiza wananchi kuendelea kutembelea mabanda ya Serikali ili kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji, biashara, mikopo na programu mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha na ustawi wa Watanzania.

spot_img

Latest articles

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

COASCO: Ukaguzi wa vyama vya ushirika waongeza uwazi na kuimarisha imani ya wanachama

Na Tatu Mohamed Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limesema ukaguzi...

More like this

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...