Mbegu bora zatatajwa kuwa msingi wa mafanikio ya kilimo biashara

Na Mwandishi Wetu

MATUMIZI ya mbegu bora yameelezwa kuwa nguzo muhimu ya kufanikisha ajenda ya kilimo biashara nchini kwa kuongeza uzalishaji wenye tija, kuimarisha usalama wa chakula na kuwezesha Tanzania kunufaika na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Nyasebwa Chimagu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo taasisi hiyo inashiriki kupitia banda la Wizara ya Kilimo.

Chimagu alisema mafanikio ya kilimo biashara yanategemea matumizi ya mbegu bora zilizothibitishwa, akieleza kuwa mbegu hizo huwasaidia wakulima kupata mavuno mengi, yenye ubora na yanayokidhi mahitaji ya soko.

“Serikali imeendelea kusisitiza kilimo biashara, na msingi wake ni matumizi ya mbegu bora. Jukumu la TOSCI ni kuhakikisha mbegu zote zinazowafikia wakulima zimehakikiwa na kuthibitishwa ubora wake,” alisema.

Alieleza kuwa TOSCI ina jukumu la kusajili aina mpya za mbegu baada ya kufanyiwa majaribio yanayothibitisha ubora wake, uwezo wa kustawi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na sifa zake za kilimo.

Aidha, taasisi hiyo husajili wazalishaji wa mbegu na mashamba ya uzalishaji, huku ikifanya ukaguzi katika hatua zote za uzalishaji kuanzia shambani hadi maabara ili kuhakikisha mbegu zinakidhi viwango vya ubora kabla ya kuingia sokoni.

“Tunafanya ukaguzi kuanzia shambani hadi maabara na kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi ili kuhakikisha mbegu zote zina ubora uliosajiliwa,” alisema.Chimagu alisema TOSCI imeanzisha mfumo wa kidijitali unaowawezesha wakulima kuthibitisha uhalali wa mbegu kabla ya kuzinunua.

Alifafanua kuwa mbegu zote halali lazima ziwe zimefungashwa na kubeba lebo rasmi ya TOSCI, akibainisha kuwa ni kinyume cha sheria kuuza mbegu ambazo hazijafungashwa.

“Mbegu zote zinazouzwa lazima ziwe kwenye vifungashio vyenye taarifa muhimu pamoja na lebo ya uthibitisho wa TOSCI. Hili ni takwa la Sheria ya Mbegu,” alisema.

Aliongeza kuwa wakulima wanaweza kuhakiki uhalali wa mbegu kwa kupiga 14852# kupitia simu za mkononi na kuingiza namba iliyo kwenye lebo ya mbegu ili kupata taarifa kama mbegu hiyo ni halisi au la.

“Ikiwa mfumo unaonyesha mbegu ni halisi, mkulima anaweza kuinunua kwa uhakika. Endapo si halisi, wananchi wanapaswa kutoa taarifa mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika,” alisema.

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa wanapobaini mbegu zenye shaka ili TOSCI iweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, Chimagu alisema Tanzania imeongeza uwezo wa kuzalisha mbegu zinazokubalika kimataifa kupitia maabara ya taifa yenye ithibati ya kimataifa, hali inayowezesha mbegu zinazozalishwa nchini kuuzwa katika masoko mbalimbali ya nje.

Alisema kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Sabasaba, TOSCI inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya mbegu bora, uzalishaji wa mbegu, biashara ya mbegu na fursa zilizopo katika masoko ya ndani na kimataifa.

Aliwahimiza wananchi, wawekezaji na wadau wa sekta ya kilimo kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu teknolojia za uzalishaji wa mbegu bora na namna ya kushiriki katika biashara hiyo, akisema hatua hiyo itachangia kuongeza tija katika kilimo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

spot_img

Latest articles

Mhitimu wa VETA abuni mashine za kuongeza thamani ya mazao, ajiajiri kupitia kampuni yake

Na Mwandishi Wetu MHITIMU wa mafunzo ya ufundi stadi kupitia VETA, Ernest Maranya, amebuni...

MHE.SALOME: WANANCHI WANAOPITIWA NA MIUNDOMBINU YA UMEME WAUNGANISHIWE HUDUMA KWA SH. 27,000

Na Mwandishi Wetu, Mara Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Serikali ya Awamu...

TTCL Yakabidhi Magari 6 ya Sh. Milioni 903 Kuimarisha Ufanisi wa Huduma

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuboresha...

Ofisi ya Usuluhishi wa Kodi Yaahidi Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi imesema, inaendelea...

More like this

Mhitimu wa VETA abuni mashine za kuongeza thamani ya mazao, ajiajiri kupitia kampuni yake

Na Mwandishi Wetu MHITIMU wa mafunzo ya ufundi stadi kupitia VETA, Ernest Maranya, amebuni...

MHE.SALOME: WANANCHI WANAOPITIWA NA MIUNDOMBINU YA UMEME WAUNGANISHIWE HUDUMA KWA SH. 27,000

Na Mwandishi Wetu, Mara Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Serikali ya Awamu...

TTCL Yakabidhi Magari 6 ya Sh. Milioni 903 Kuimarisha Ufanisi wa Huduma

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuboresha...