Kamati ya uratibu ya Mradi wa SOFF yakutana jijini Dodoma

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), walifanya kikao kazi cha tano cha Kamati ya Uratibu wa Mradi wa SOFF (Systematic Observations Financing Facilit) katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Kikao hicho kiliwakutanisha wataalamu muhimu ili kupitia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SOFF na kujadili vipaumbele vya kimkakati kwa mwaka 2026, vinavyolenga kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mradi.

Majadiliano yalijikita katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2026, ufuatiliaji na tathmini ya mradi, pamoja na shughuli za mawasiliano na uhamasishaji zilizopangwa kwa mwaka 2026.

Kamati pia ilipitia maamuzi na maelekezo kutoka kikao cha Tatu cha Kamati Tendaji ya Mradi wa SOFF kilihofanyika Aprili 2026.

Wakizungumza katika ufunguzi, Wenyeviti wenza wa kamati hiyo, Dkt. Paschal Waniha kutoka TMA na Dkt.Abbas Kitogo kutoka UNDP, walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa wakati katika shughuli zote zilizopangwa za mradi wa SOFF Tanzania.

Aidha,kikao kilihitimishwa kwa wajumbe kutoa dhamira ya pamoja ya kuimarisha uratibu, kuharakisha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa, na kuongeza ufanisi wa jumla wa mradi wa SOFF nchini Tanzania.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this