TTB yaeleza Utalii wa michezo unavyochangia uchumi wa jamii

Na Mwandishi Wetu, Njombe

BODI ya Utalii Tanzania (TTB), imesema utalii wa michezo umeendelea kuwa nguzo muhimu ya kuongeza mapato kwa jamii zinazozunguka Hifadhi za Taifa, huku wananchi wa maeneo hayo wakinufaika kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na ongezeko la wageni.

Hayo yameelezwa Mei 2, 2026 wakati wa mbio za Kitulo Garden Marathon mkoani Njombe, ambapo wananchi kutoka maeneo ya jirani walijitokeza kwa wingi kufanya biashara mbalimbali, hatua inayochangia kuongeza kipato chao na kupunguza utegemezi wa shughuli zisizo rasmi ikiwemo ujangili ndani ya hifadhi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TTB, Ephraim Mafuru, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Ashatu Kijaji, amesema mbali na kukuza utalii wa michezo, marathon hiyo imewezesha wananchi wengi kujipatia kipato kupitia huduma mbalimbali zikiwemo malazi, vyakula, vinywaji, usafiri pamoja na uuzaji wa kazi za mikono.

“Tumeshuhudia namna ambavyo wananchi wamenufaika moja kwa moja kupitia tukio hili. Hii inaonyesha wazi kuwa utalii ni sekta jumuishi inayogusa maisha ya watu wengi,” amesema Mafuru.

Aidha, amesema marathon hiyo pia imerejesha manufaa kwa jamii kwa kutoa kompyuta 40 zitakazogawiwa katika shule nane za sekondari za Wilaya ya Makete.

Mafuru ameeleza kuwa tukio hilo limebeba mambo manne muhimu ambayo ni kukimbia, kutangaza utalii, kuhifadhi mazingira na kusaidia jamii.

“Unakimbia, unatangaza, unahifadhi lakini pia unasaidia jamii. Hali hii itaongeza ushiriki wa wananchi katika uhifadhi wa maliasili,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA na Mkuu wa Kanda ya Kusini, Godwell Ole Meing’ataki, amesema tukio hilo limefungua fursa kwa wajasiriamali na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo.

Ameongeza kuwa zaidi ya washiriki 300 walioshiriki katika marathon hiyo wamechangia kuongeza mapato ya serikali kupitia ada za ushiriki na shughuli nyingine za kiuchumi zinazozunguka tukio hilo.

Naye Mratibu wa marathon hiyo, Monny Luvanda, amesema lengo la mbio hizo ni kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi, kuitangaza Hifadhi ya Taifa Kitulo pamoja na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Makete na maeneo ya jirani.

Kitulo Garden Marathon ilihusisha mbio za kilomita 5, 10 na 21, zilizovutia washiriki wengi na ushindani mkubwa.

Washindi mbalimbali walizawadiwa zawadi tofauti, huku washindi watatu wa kwanza wakipata fursa ya kulala na kutalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo pamoja na wenza wao kwa siku mbili.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...