Tume yataja idadi waliopoteza maisha matukio ya Oktoba 29, Dar yaongoza

Na Mwandishi Wetu

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema kuwa jumla ya watu 518 walipoteza maisha katika ghasia zilizotokea kipindi hicho.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya ripoti ya uchunguzi kwa Rais Samia Suluhu Hassan leo Aprili 23, 2026, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Chande amesema kati yao wanaume walikuwa 490 sawa na asilinia 94.6, wanawake wakiwa 28 sawa na asilimia 5.4.

Amesema kati ya vifo hivyo, watoto walikuwa 21, ambapo 15 walikuwa na umri wa miaka 15-17, wanne umri wa miaka 7-10, wawili chini ya miaka mitano.

Amefafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam uliongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo, ukirekodi watu 182. Mwanza vifo 90, Mbeya vifo 80 na Arusha vifo 53.



“Vifo 205 sawa na asilimia 96.7 vilikuwa vya raia na vifo 16 asilimia 3.1 ni vya maafisa na askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, kati ya watu 518 waliofariki, watu 373 walifikishwa hospitali wakiwa wamefariki, huku 121 walifariki wakati wanapata matibabu katika hospitali na maiti 24 hazina taarifa kamili,”ameeleza Jaji Chande.

Amebainisha kuwa kati ya maiti 518, maiti 480 sawa na asilimia 92.7 zilitambuliwa na kuchukuwa na familia zao kwa ajili ya taratibu za mazishi, huku maiti 260 pekee ndizo zilizofanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Sababu kubwa ya kutofanyika uchunguzi kwa maiti zilizobaki ilikuwa ni kukosekana kwa ridhaa kutoka kwa ndugu na familia. Familia nyingi ziliomba kuchukua miili ya wapendwa wao kwa haraka ili kuwahi taratibu za mazishi, jambo lililozuia taratibu za upasuaji wa kitabibu kufanyika,”

Kwa mujibu wa Jaji Chande matokeo ya uchunguzi wa kisayansi kwa maiti, miili mingi ilionyesha kuwa na majeraha ya kutobolewa na vitu vyenye ncha kali, kuwepo kwa mivunjikokatika sehemu mbalimbali, ambapo majeraha hayo yalisababisha kupoteza damunyingi, hali iliyokuwa chanzo kikuu cha vifo hivyo

Hata hivyo, maiti 21 hazikuonyesha aina yoyote ya majeraha ya nje, huku maiti sita (6) zikikutwa na majeraha yaliyosababishwa na moto.

Jaji Chande amesema kuwa takwimu hizo zinaonesha uzito wa athari za ghasia hizo na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia matukio kama hayo kujirudia katika chaguzi zijazo.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...