Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua inayotajwa kuwa ni muendelezo wa juhudi za makusudi za kupanua wigo wa ajira kwa vijana na kuwajengea uwezo wa kushiriki katika uchumi wa kimataifa.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana hao iliyofanyika Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, alisema kuwa mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza ajira na kuwawezesha vijana kiuchumi.

Alieleza kuwa Serikali imeendelea kufungua na kuimarisha njia salama za uhamiaji wa nguvu kazi kwa kushirikiana na nchi rafiki pamoja na taasisi za kikanda na kimataifa, ili kuhakikisha Watanzania wanapata ajira zenye staha huku haki zao zikilindwa.

“Tunawahakikishia vijana wetu kuwa wanakwenda kufanya kazi katika mazingira salama na yenye kulinda utu wao. Serikali ipo pamoja nao katika kila hatua,” alisema Sangu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ajira, Jane Sologo, aliwashukuru mawakala binafsi kwa mchango wao mkubwa katika kuwaunganisha Watanzania na fursa za ajira nje ya nchi, akibainisha kuwa ushirikiano huo umeongeza ufanisi katika sekta ya ajira.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala Tanzania, Abdallah Khaled Mohamed, aliipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau hao, akisema hatua hiyo imeongeza uaminifu na uwazi katika mchakato wa ajira za nje.

Akitoa mtazamo wa sekta binafsi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UCDP Tanzania, Patrick Kawogo, alisema vijana hao wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi ni rasilimali muhimu inayoweza kuchangia maendeleo ya taifa kupitia uzoefu na kipato watakachokipata.

Alifafanua kuwa kampuni yao imekuwa ikiunganisha vijana na fursa za ajira na mafunzo ya vitendo katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani, Canada na nchi za Scandinavia kama Ujerumani, Norway, Denmark na Uholanzi.

“Tunaunganisha vijana na ajira pamoja na mafunzo ya muda wa mwaka mmoja na zaidi katika sekta mbalimbali kama kilimo, utalii na ukarimu (hospitality), pamoja na uhandisi. Hii imekuwa fursa kubwa kwa vijana wa Kitanzania hasa katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira nchini,” alisema Kawogo.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...