Lukuvi afariki dunia

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (70) amefariki dunia saa 1:00 asubuhi ya leo Jumatano, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kifo hicho kimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka juu ya msiba huo wa Lukuvi aliyezaliwa Agosti 15, 1955.

Taarifa hiyo imeeleza Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isiman, Mkoa wa Iringa amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

“Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo,” amesema Dk Kusiluka.

Lukuvi alikuwa miongoni mwa wabunge waandamizi bungeni ambaye amekuwa mbunge wa Ismani kuanzia mwaka 1995 hadi sasa akihudumu kwa zaidi ya miaka 30.

spot_img

Latest articles

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

MD Twange aeleza kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa mradi wa Hale

📍Ni ule wa kuboresha kituo cha kufua umeme 📍Amuagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa...

Rio Ferdinand avutiwa na Tanzania, kuitupia jicho Serengeti Boys

Na Winfrida Mtoi NYOTA wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, ameeleza jinsi alivyovutiwa na...

More like this