Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu 

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini Dar es Salaam kutumika kwa  mechi za  Ligi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo  leo Januari 29, 2026, imesema  miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu.

“Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF,” imesema taarifa hiyo.

Aidha TFF imezikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.

Miongoni mwa timu zinazotumia uwanja huyo kama uwanja wake wa nyumbani katika mechi za Ligi ni Yanga, Tausi Queens na wenyeji KMC.

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Al Ahly yaanza safari kuifuata Yanga Zanzibar

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imeanza safari kuelekea Zanzibar kwa...

More like this