Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga, utakaochezwa Jumamosi Januari 31, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini, Yanga ilipoteza kwa mabao mawili, hivyo wanajangwani hao wanatakiwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani ili kujiweka nafasi nzuri ya kufuzu hatua nyingine.
Msimamo wa kundi B la michuano hiyo, Al Ahly inaongoza ikiwa na pointi saba, Yanga inafuatia na pointi nne, huku AS FAR na Kabylie kila mmoja akiwa na alama mbili katika michezo mitatu timu hizo zilizocheza.


