2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu

MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina, huku mageuzi katika mashirika ya umma yakiendelea kuonesha matokeo chanya kwa wingi.

Katika kipindi hiki, thamani ya uwekezaji wa Serikali iliongezeka hadi kufikia Sh92.3 trilioni Juni 2025, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi yalifikia Sh1.028 trilioni, uzinduzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (PIMS) ulifanyika mwezi Agosti, na Serikali ilinunua hisa ya asilimia 10 katika Benki ya Ushirika ya Tanzania.

Aidha, idadi ya kampuni za madini ambapo Serikali ina hisa pia iliongezeka kutoka 4 hadi 12, huku bodi za wakurugenzi zikiongezeka, na viongozi wakuu 114 wakishiriki mafunzo ya uongozi na usimamizi.

Vilevile, OMH iliibuka mshindi wa pili – tuzo za Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha 2024 (Kundi la Idara za Serikali Zinazojitegemea) kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Pamoja na mafanikio hayo, mwaka huu umeacha kumbukumbu mbaya kwani OMH ilimpoteza Afisa Hesabu Mkuu Daraja la 1, Bi Miriam Mnzava, ambaye alifariki Novemba 28.

Kuongeza thamani ya uwekezaji wa serikaliThamani ya uwekezaji katika mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache iliongezeka kutoka Sh86.3 trilioni hadi Sh92.3 trilioni kufikia Juni 2025.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema kuwa ongezeko hili linatokana na utendaji bora, uwajibikaji, na mageuzi ya kiutendaji katika mashirika, na kampuni 308 ambazo Serikali ina hisa chache.

Kuongeza mapato yasiyo ya kodiOngezeko la uwekezaji katika mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache liliambatana na ongezeko la kihistoria la mapato yasiyo ya kodi, yaliyofikia Sh1.028 trilioni kufikia Juni 2025 (mwaka wa fedha 2024/25).

Hili ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2024 na asilimia 34 zaidi ya makusanyo yote ya mwaka wa fedha 2023/24. Kiasi hicho, alisema Mchechu, kinahusisha Sh603.4 bilioni kama gawio, Sh363.4 bilioni kama michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi, huku Sh61 bilioni ikiwa ni mapato mengine.

Ongezeko la makusanya ya mapato yasiyo ya kodi ni matokeo ya mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Uzinduzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (PIMS)Agosti 2025, OMH ilizindua rasmi Mfumo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (PIMS), ulioanzishwa ili kurahisisha ufuatiliaji wa papo kwa papo wa mashirika ya umma na uwekezaji wa Serikali.

Uzinduzi ulifanyika kwenye Mkutano wa Wakuu wa Taasisi na Wenyeviti wa Bodi (CEOs Forum 2025), jijini Arusha, na kuhudhuriwa na wakuu wa taasisi za umma na wenyeviti wa bodi zaidi ya 650, ukiashiria hatua kubwa katika uwazi, ufanikishaji wa maamuzi ya kisera, na ufuatiliaji wa wa mali za umma.

Uwekezaji katika benki ya Ushirika ya TanzaniaSerikali pia ilichukua hatua za kimkakati katika sekta ya kifedha kwa kununua asilimia 10 ya hisa katika Benki ya Ushirika ya Tanzania.Benki hii ilizinduliwa rasmi Aprili 28, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Msajili wa Hazina,alikabidhi hundi ya Sh5.8 bilioni kuashiria uwekezaji wa Serikali. Benki yenye mtaji wa Sh58 bilioni ina umiliki mchanganyiko: vyama vya ushirika asilimia 51, CRDB Bank asilimia 20, wawekezaji binafsi asilimia 19, na OMH asilimia 10. Hatua hii inalenga kuondoa mapengo ya kifedha katika kilimo na vyama vya ushirika.

Kuongeza ushiriki wa serikali katika kampuni za madini Idadi ya kampuni za madini ambazo Serikali ina hisa iliongezeka kutoka 4 hadi 12, ikionyesha ongezeko la asilimia 200, huku Ofisi ikiwa mbioni kusaini mikataba 10 mipya.

Hatua hii inalenga kuhakikisha rasilimali za nchi zinanufaisha wananchi wa Tanzania na Taifa kwa ujumla. Kuimarisha utendaji wa mashirika ya umma na bodi za wakurugenziOMH iliimarisha utendaji wa mashirika ya umma kupitia viashiria muhimu vya utendaji (KPIs) na tathmini za bodi za wakurugenzi.

Idadi ya taasisi zisizo na bodi ilipungua kutoka 52 mwaka 2019/20 hadi 28 mwaka 2024/25. Mabadiliko haya yameimarisha uwajibikaji, uwazi, na ubora wa maamuzi katika mashirika ya umma.

Mafunzo Wakuu wa taasisi 114 walishiriki mafunzo ya awali ‘CEO Induction Programme’ Julai 2025, yaliyojikita katika mbinu za kisasa za usimamizi, uwajibikaji, uwazi, na utoaji wa huduma bora. Kwa mara ya kwanza mafunzo haya yaliyofanyika kwa kushirikiana na Taasisi ya UONGOZI, Oktoba 2024, yaliwanufaisha wakuu wa taasisi 111, huku lengo likiwa ni kuimarisha uwezo wa viongozi katika utekelezaji wa sera za taifa.

KutambuliwaMwaka 2025 umeacha alama muhimu kwa OMH kwani iliibuka mshindi wa Pili – tuzo za Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha 2024 (Kundi la Idara za Serikali Zinazojitegemea) kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hiyo ilikabidhiwa usiku wa Alhamisi, Disemba 4, 2025, jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, ikiwa ni sehemu ya kutambua taasisi zinazozingatia viwango, weledi na uwazi katika uandaaji wa taarifa za fedha za mwaka.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Hassan Mohamed, alisema mafanikio hayo yametokana na uandaaji mzuri wa taarifa za kihesabu kwa kufuata miongozo na kanuni.

Aidha, alisema, hilo lisingewezekana bila kujituma kwa watumishi pamoja na uongozi madhubuti wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu.

Hata hivyo, mwaka wa 2025 pia uliacha pigo kubwa kwa OMH kufuatia Kifo cha Miriam Mnzava, Afisa Hesabu Mkuu Daraja la 1 kutoka Kurugenzi ya Fedha na Uhasibu.

Miriam ambaye alifariki Novemba 28, 2025 mkoani Morogoro, atakumbukwa kwa ufanyaji kazi kwa juhudi na maarifa.

spot_img

Latest articles

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...

Serikali yawekeza zaidi ya Sh. Bilioni 280 kuimarisha upatikanaji umeme Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano...

More like this

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...