Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na kuharibu magari mawili yaliyotumika kusafirishia mwili wa marehemu, tukio lililofanywa na waombolezaji wa msiba wakidaiwa kutilia mashaka mazingira ya kifo cha marehemu.

 Tukio hilo limetokea jana Disemba 17, 2025 katika Wilaya ya Mvomero mkoani humo Kitongoji cha Kilingeni, Kijiji cha Lusanga, Kata ya Diongoya, Tarafa ya Turiani.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro iliyotolewa leo  Desemba 18,2025 imeyataja magari hayo kuwa ni Mazda CX-5 yenye namba T.214 EJU na Toyota Noah yenye namba T.350 DCH.

“Magari hayo yalitumika kusafirisha mwili wa marehemu Mwanahasan Juma Hamis (18) ambaye ni mfanyakazi wa ndani aliyefariki kwa maradhi jijini Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa shughuli za mazishi,” imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakati shughuli za mazishi zikiandaliwa ilitokea taharuki iliyohusishwa na kutiliwa mashaka ya mazingira ya kifo cha marehemu hali iliyosababisha kuchomwa ndani kwa magari hayo na kuwafungia ndani wasindikizaji wa msiba ili watoe maelezo zaidi.

Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwaokoa wasindikizaji wa msiba waliofungiwa kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mtaa na kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya kifo hicho.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na una madhara makubwa

spot_img

Latest articles

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na...

CRDB yashirikiana na Kids’ Holiday Festival kukuza elimu ya fedha kwa watoto

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival...

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

More like this