CRDB yashirikiana na Kids’ Holiday Festival kukuza elimu ya fedha kwa watoto

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival kwa lengo la kuandaa matamasha ya watoto yatakayolenga kuwawezesha kukuza maarifa katika masuala ya fedha, uwekezaji na akiba, hatua inayolenga kujenga msingi imara wa ujumuishi wa huduma za kifedha kuanzia ngazi za awali.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili, amesema ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kutoa elimu ya fedha kwa vijana na kuongeza ujumuishi wa huduma za kifedha katika jamii.

Amesema kupitia matamasha hayo, watoto watapata fursa ya kujifunza kuhusu nidhamu ya fedha kwa njia rafiki, ya kuburudisha na inayoeleweka kirahisi.

“Ushirikiano huu ni mchango wetu katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kifedha ya kidijitali, huku tukiwajengea watoto misingi ya utunzaji na usimamizi wa fedha tangu wakiwa wadogo,” amesema Adili.

Sambamba na udhamini huo, Benki ya CRDB imetangaza kutoa ufadhili wa masomo kwa washindi wanne watakaopatikana katika matamasha mawili yatakayofanyika Disemba 20, 2025 jijini Dar es Salaam na Disemba 27, 2025 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kids’ Holiday Festival, Geraldine Mashele, ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali kushirikiana na tamasha hilo, akisema ushirikiano huo utawezesha kufikisha elimu ya fedha kwa watoto kwa njia bunifu, rafiki na inayochochea uelewa wa haraka.

“Kwa kushirikiana na CRDB, tunaamini watoto watajifunza umuhimu wa akiba, uwekezaji na matumizi sahihi ya fedha kwa vitendo kupitia michezo na burudani mbalimbali,” amesema Mashele.

Kupitia ushirikiano huo, jamii imetakiwa kuongeza uelewa kwa watoto kuhusu mnyororo wa huduma za kifedha, hatua inayotajwa kuwa chachu ya ujumuishi wa huduma hizo pamoja na kuimarisha uhimilivu wa uchumi wa taifa kwa ujumla.

spot_img

Latest articles

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

Rais Mwinyi: SMZ kuendelea kushirikiana na TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...

Tanzania yajumuishwa kwenye orodha ya Nchi zenye vikwazo vya kuingia Marekani

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitisha kuwa Serikali ya...

More like this

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

Rais Mwinyi: SMZ kuendelea kushirikiana na TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...