Watanzania waaswa kudumisha amani, Umoja na mshikamano

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika, Watanzania wametakiwa kukumbuka siku hiyo kwa misingi ya haki, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa, huku wakiepuka mivutano yoyote inayoweza kugawanya taifa, ikiwemo migawanyiko ya kidini, kikabila au kisiasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Everlasting Legal Aid Foundation, Dkt. Khamis Masoud, amesema kuwa kumbukizi ya uhuru inapaswa kuwa fursa ya kuimarisha mshikamano na kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao.

Dkt. Masoud amesema ni muhimu viongozi wa dini na serikali kuungana katika kuhubiri amani, heshima na ustahimilivu, kwa kuwa wao ni nguzo muhimu katika kuunganisha jamii.

“Ni muhimu viongozi wa dini kutazama namna bora ya kuwaleta wananchi pamoja kuhusu amani badala ya kufanya mambo yanayoweza kugawanya taifa kwa mitazamo ya kidini,” amesema Dkt. Masoud.

Aidha, amesisitiza kuwa viongozi wa serikali wanapaswa kuwa wazalendo na wenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa.

Ameongeza kuwa hata pale ambapo ni lazima, viongozi hao wanapaswa kuwa tayari kung’atuka madarakani ili kulinda amani, mshikamano na haki nchini.

Mbali na hayo, Dkt. Masoud amebainisha umuhimu wa kuimarisha diplomasia na mahusiano ya kimataifa, akieleza kuwa Tanzania inahitaji uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali ili kuendeleza maendeleo na uchumi wa nchi.

Ameitaka serikali kuendelea kumuunga mkono Rais katika utekelezaji wa mikakati ya kidiplomasia yenye manufaa kwa taifa.

Itakumbukwa kuwa kwa mwaka 2025, serikali iliahirisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika, na kuelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kutumika katika sherehe hizo kufadhili ukarabati wa miundombinu iliyoathiriwa na vurugu za uchaguzi mkuu zilizotokea Oktoba 29, 2025.

spot_img

Latest articles

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

📌Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini 📌Mradi utakuwa...

NDEJEMBI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA SHILINGI BILIONI 204.7 WA MRADI WA UMEME WA JUA WA MEGAWATI 100 KISHAPU

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi, leo Julai 27, 2026, ameshuhudia...

DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Na Mwandishi Wetu KUFUATIA kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini...

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

More like this