Uwanja wa Mkwakwani wafungiwa

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeufungia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za  mchezo huo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 26, 2025 na shirikisho hilo, imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu.

“Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.

“TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja,” imeeleza taarifa hiyo.

Mechi ya mwisho katika uwanja huo imechezwa leo ya Ligi Kuu Bara ambapo wenyeji Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Uamuzi wa kuufungia uwanja huo umekuja muda mchache baada ya kumalizika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo wenyeji Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City. Timu nyingine inayotumia uwanja huo ni African Sports ya Ligi ya Championship.

spot_img

Latest articles

ETDCO yaahidi kukamilisha Mradi wa Umeme katika vitongoji 372 Ruvuma kwa wakati

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji...

Wadau sekta ya Hali ya Hewa wajadili utabiri wa Masika 2026

Na Mwandishi Wetu WADAU kutoka sekta mbalimbali nchini wamekutana kujadili utabiri wa msimu wa...

WMA yafunga Mtambo wa kisasa unaohakiki Dira za Maji Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Vipimo (WMA) umesimika mtambo wa kisasa wa kidijitali wa...

Benki ya CRDB yaja na ‘Benki Kimpango Wako’ yaahidi huduma bora zaidi mwaka 2026

Na Mwandishi wetu BENKI ya CRDB imezindua kampeni yake ya mwaka 2026 inayoitwa ‘Benki Kimpango...

More like this