Watuhumiwa 57 wa uhaini waachiwa huru

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Ilemela imewaachia huru watuhumiwa 57 kati 61 wa kesi ya uhaini waliokuwa wakishikiliwa kufuatia  maandamano na matukio ya vurugu za baada ya uchaguzi yalitokea kuanzia Oktoba 29, 2025.

Uamuzi wa kufuta mashtaka hayo umetolewa leo Novemba 24,2025 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Stella Kiama, katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela iliyopo kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Buswelu.

Hatua hiyo imetokana na  upande wa mashtaka, kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Safi Amani, kuwasilisha ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) la kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Shauri hilo namba 26641/2025 limeletwa kwa ajili ya kutajwa kwa mara ya pili mahakamani hapo leo ambapo kwa mara ya kwanza lilitajwa Novemba 24, 2025.

Vijana hao ni miongoni mwa wale waliokuwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi na baadaye kufikishwa Mahakamani wakidaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kwenye maandamano yaliyozaa vurugu zilizopelekea uharibifu wa mali, majeruhi na vifo.

spot_img

Latest articles

TCAA YAIMARISHA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA DAWATI MAALUM

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia kwa Mkurugenzi wake...

TBA YASHINDA TUZO YA BANDA BORA SABASABA, YATANGAZA DIRA YA KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umeibuka mshindi wa pili na kutunukiwa tuzo...

VETA yajivunia ushindi, yaeleza mchango wa Mafunzo ya Ufundi Stadi

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema ushindi...

Twange: Tanesco yazidi kupanua Nishati Safi ya kupikia, kuimarisha usambazaji wa umeme Zanzibar

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange, amesema Shirika...

More like this