Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi wa Kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambapo kwa ushindi huo anaenda kuwa Spika wa tisa wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zungu ameibuka mshindi na kutangazwa hii leo Novemba 11, 2025 kwa Kupata Kura 378 dhidi ya wapinzani wake Veronica Charles Tyeah ambaye hajapata kura kutoka chama cha NFA, Anitha Alfan aliyepata kura moja kutoka chama cha NLD, Ndoge Said Ndonge aliyepata Kura moja kutoka chama cha AAFP pamoja na Amin Alfred Yango ambaye hajapata kura kutoka chama cha ADC.

Zungu amekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 20 ambapo aliingia bungeni rasmi mwaka 2005.

Kwa kipindi hicho amekuwa Mwenyekiti wa Bunge 2012-2021 na Naibu Spika 2022 mpaka 2025.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this