Jaji Mwambegele Akagua Maandalizi ya Vituo Maalum vya Kupigia Kura Wilayani Tanganyika

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ametembelea na kujionea maandalizi ya ujenzi wa vituo 83 kati ya 90 vya Wapiga Kura vilivyotengwa maalum kwaajili ya wakazi wa zilizokuwa Kata za Ilangu, Ipwaga, Bulamata na Mishamo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ambazo zilifutwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287.

Jaji Mwambegele alitembelea eneo hilo la Kata ya Tongwe katika Kitongoji cha Luhafwe leo Oktoba 26, 2025 akiwa ameambatana na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Katavi, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanganyika na watendaji wengine wa uchaguzi kuangalia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.

Akizungumza akiwa katika eneo la Mnada wa Kitongoji cha Luhafwe, Jaji Mwambegele alisema Tume ilitangaza kuhamisha baadhi ya vituo nje ya Makazi ya Wakimbizi hivyo amefika na kuangalia maandalizi hayo na Tume imetoa matangazo katika maeneo yaliyofutwa na imeweka vituo maeneo jirani.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika, Kagemlo Mutagwaba amesema wapiga kura kutoka kata zilizofutwa wamehamasishwa na wameonesha utayari wa kujitokeza kupiga Kura katika maeneo mapya yaliyotengwa.

Watanzania wanatarajia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 29, 2025 huku kauli mbiu ikiwa ni ‘Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura’.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...