Yanga yakiri vita ya kupambana na jezi feki ngumu

Na Winfrida Mtoi, The Media Brains

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umekiri kuwa vita ya kudhibiti jezi feki ni ngumu pamoja na jitihada wanazofanya na kutumia mbinu nyingi lakini imeshindikana, walichofanikiwa ni kupunguza madhara na si kukomesha suala hilo.

Hayo yamezungumzwa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe leo Septemba 26, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa jezi mpya toleo la pili ya timu hiyo.

“Vita ya jezi feki sio vita nyepesi, ni vita ngumu mmno, ni vita nzito kupambana nayo, tumetumia mbinu nyingi, tulichofanikiwa ni kupunguza madhara lakini hatujafanikiwa kukomesha tatizo hilo.

Jezi mpya ya Yanga iliyozinduliwa leo

“Sisi tumezindua jezi hivi karibuni na mzigo wetu tulioleta msimu huu umeisha, lakini cha ajabu bado tunaendelea kupewa taarifa kuwa mizigo mikubwa ya jezi bado inaendelea kuingia nchini. Ila uongozi wa Yanga umekuja mpango wa kukomesha hili mwaka huu. Naamini njia tuliyokuja nayo hii itakuwa ni komesha,” amesema Kamwe.

Ameeleza kuwa wamedhamiria kupambana na hata toleo hilo jipya ni moja ya suluhisho kwa kuwa hawawezi kuona klabu inazidi kupoteza mapato na kuwanufaisha wengine.

Hivi karibuni uongozi wa Klabu ya Simba nao ulitoa taarifa za uwepo wa jezi feki zinazouzwa katika mikoa mbalimbali kama vile Morogoro, Singida, Geita na Mwanza.

Mwaka 2023 Ofisa Habari wa Yanga, Kamwe  aliongoza zoezi la kukamata jezi feki za Yanga na Simba kwenye godauni moja maeneo ya Mbozi Road, Temeke, Dar Es Salaam zilizokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya sh. 10 bilioni.

spot_img

Latest articles

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

More like this