Kocha Simba aaga, atangazwa Raja Casablanca

Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameaga rasmi wadau na mashabiki wa klabu hiyo na tayari ametangazwa klabu yake ya zamani ya Raja Casablanca ya nchini Morocco kukinoa kikosi hicho.

Raja Casablanca leo Septemba 22, 2025 imetoa taarifa ya mabadiliko ya benchi lake la ufundi na kumtangaza Fadlu ambaye aliwahi kutumika kama kocha msaidizi, kuwa Kocha Mkuu.

Kocha huyo hakuonekana wakati Simba ikirudi kutoka Botswana ilipokwenda mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.

Fadlu aliyedumu Simba kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili, ameaga muda mfupi baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa kocha huyo ameachana na timu hiyo, licha ya uongozi wa Simba kushindwa kutoa  taarifa rasmi hadi sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Fadlu ameandika walaka wa kuaga Simba unaosema: “Ni kwa moyo mzito naiaga Simba. Tangu nilipowasili, nilihisi shauku ya klabu hii kubwa na upendo wa mashabiki wake wa ajabu. Kwa pamoja tulipigana, kusherehekea, na kuimarika kupitia kila ushindi na kila changamoto.

Shukrani zangu za dhati kwa Rais Mo Dewji kwa uongozi wake wa kutia moyo, maono, na msaada wake wa kila mara.

Kwa wachezaji: endelea kupigana, endelea kuamini, na endelea kuinua beji kwa heshima. Kwa wafanyikazi na wasimamizi: asante kwa uaminifu wako na kujitolea bila kuchoka nyuma ya pazia.

Kwa mashabiki wa Simba: Wewe ndiye mapigo ya moyo wa klabu hii. Sauti zako, nyimbo zako, shauku yako isiyoyumba zitasikika katika kumbukumbu yangu. Asante kwa kukaribisha familia yangu kama yako.

Simba daima itakuwa sehemu yangu, na ninaitakia klabu mafanikio, mafanikio na vikombe mbeleni. Asanteni Sana, forever Nguvu Moja ,”

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...