Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waridhishwa na kasi ya utekelezaji Bwawa la Kidunda

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, mkoani Morogoro huku wakisema wana nafasi ya kushauri na kusaidia mambo mbalimbali yakiwemo ya kimkataba.

Mradi wa Kidunda unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 335, unatarajia kukamilika ifikapo Juni 2026 na kuchangia kuimarisha huduma ya maji mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuzalisha umeme megawati 20 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya taifa.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kisamo Fredrick ameongoza ujumbe wa ofisi hiyo kutembelea mradi huo akisema, wao wana nafasi kubwa katika miradi ya kimkakati na kimaendeleo kushauri na kusaidia mambo mbalimbali yakiwemo ya kimkataba ili kuhakikisha miradi inakwenda bila kukwama.

“Niwashukuru DAWASA, wamekua wakitushirikisha mara kwa mara, nafasi yetu ni kupitia maswala mbalimbali katika miradi na kuzuia changamoto zinazoweza kukwamisha miradi kutokea na kusaidia kusukuma miradi iweze kukamilika kwa wakati,” amesema Kisamo.

Amesema changamoto zilizobainishwa katika utekelezaji wa mradi huu wamezipokea na kwa nafasi yao watashirikiana na wizara zinazohusika kuhakikisha mradi huu haukwami ili uweze kuleta tija.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi kutoka DAWASA, Mhandisi Christian Christopher ameshukuru ujumbe huo kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutembelea na kusikiliza changamoto zinazokabili.

“Ukaribu wao kwetu ni muhimu sana kwani wanatusaidia kubaini viashiria mbalimbali vinavyoweza kuleta shida na kufanya mradi usitekelezeke kwa wakati. Haya yote waliotushauri tunayapokea kwa uzito mkubwa na kuanza kuyafanyia kazi mara moja,” amesema Mhandisi Christopher.

spot_img

Latest articles

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

DCEA yakamata Tani 9.93 za Dawa za Kulevya, Watuhumiwa 151 Watiwa Mbaroni

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata tani...

Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo...

Msajili wa Hazina afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Lifezone Metal

Na Mwandishi wa OMH Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amefanya mazungumzo na Bw. Keith Liddell,...

More like this