INEC yamteua Mpina kugombea Urais

Na Winfrida Mtoi

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imemteua rasmi  Luhaga Mpina kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama Cha ACT Wazalendo katika uchaguzi  mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mpina ameteuliwa pamoja na mgombea mwenza wake, Fatma Abdulhabib  Ferej, ambapo leo Septemba 13, 2025 walifika katika Ofisi Ndogo za INEC  na  kukabidhiwa  fomu ya uteuzi na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele.

Katika tukio hilo, Mpina aliambatana na viongozi mbalimbali waandamizi wa chama hicho pamoja na wafuasi waliokuwa wakishangilia hatua ya chama chao kufanikisha uteuzi huo.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza mbele ya viongozi wa ACT Wazalendo.
Baadhi ya viongozi wa ACT Wazalendo wakiwa katika uteuzi wa mgombea Urais wa chama chao

Akizungumzia uteuzi huo, Mpina amesema hatua ya INEC kuwateua rasmi inaashiria kuwa safu yao imekamilika na watashirikiana kuhakikisha wanatumia siku za kampeni zilizobaki kufikia majimbo yote ya Tanzania.

Mpina amerejesha  fomu ikiwa ni siku mbili baada ya kushinda kesi ya kupinga kuenguliwa  kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

spot_img

Latest articles

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

More like this

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...