Mahakama kuamua hatma ya Lissu Jumatatu

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu,  amerejeshwa mahabusu leo na anatarajiwa kurejea  Jumatatu Septemba 15, 2025 kwa ajili ya Mahakama  kutoa uamuzi juu ya mapingamizi aliyowasilisha kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili.

Kesi hiyo imesikilizwa  siku nne mfululizo tangu Jumatatu katika Mahakam Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dustan Nduguru akisaidiana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Tayari Lissu amekamilisha mawasilisho ya mapingamizi yake leo Septemba 11, 2025, madai ya msingi ikiwa ni mchakato wa kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu ulikuwa na makosa mengi na kutaka kesi ifutwe, aachiwe huru, hivyo kinachosubiriwa ni uamuzi kutoka kwa jopo la Majaji watatu.

Iwapo Mahakama Kuu itakubaliana na hoja za Lissu, kesi hiyo inaweza kufutwa rasmi, endapo hoja zikikataliwa basi itaendelea kusikilizwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema wakati dunia itakuwa inaadhimisha Siku ya Demokrasia, kwao itakuwa tofauti kwani watakuwa mahakamani kujua hatma ya kesi ya Mwenyekiti wao.

spot_img

Latest articles

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

More like this

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...