Na Mwandishi Wetu
Kocha wa timu ya Taifa ya soka kwa watu wenye Ulemavu Tanzania ‘Tembo Warriors’, ameomba sapoti kutoka kwa Watanzania kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAAF), inayofanyika nchini Burundi.
Tembo Warriors ambayo tayari imewasili nchini humo, inatarajia kurusha karata yake ya kwanza kesho September 9, 2025 dhidi ya Kenya.
Mapunda amesema wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano hayo, huku akiwataka watanzania waliopo nchini Burundi kujitokeza uwanjani kusapoti timu hiyo katika kupambania ubingwa wa mashindano hayo.
“Kwa Asilimia 95% tuko tayari kwa ajili ya mchezo kikubwa tunaomba sapoti ya watanzania waliopo nchini Burundi kuja uwanjani na watanzania waliopo Tanzania kwa dua ili turudi na ubingwa, “amesema Mapunda.