Mradi wa umeme Chalinze – Dodoma wamtibua Dk. Biteko

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amekasirishwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Zuzu Dodoma ambao uliopaswa kufikia asilimia 31 lakini kwa sasa umefikia asilimia 24 tangu tangu ulivyozinduliwa Novemba mwaka 2024.

Hali hiyo ya kusuasua kwa mradi imebainika wakati Dk. Biteko alipofanya ukaguzi mradi huo katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Agosti 20, 2025.

Kutokana na hali hiyo Dk Biteko amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya TBEA ya China kuhakikisha kuwa anafidia muda wa kazi uliopotezwa wa asilimia saba ili mradi ukamilike kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini.

Novemba, 2024 Serikali ilikubaliana na mkandarasi kuwa mradi huo ufanyike ndani ya miezi 19 tu badala ya miezi 22 kwani wakati mradi unazinduliwa tayari kazi kubwa za awali zilikuwa zimeshafanyika ikiwemo za upembuzi yakinifu na utoaji wa maeneo.

“ Leo ni miezi saba imepita tangu tuzindue mradi sawa na asilimia 32 ya muda wote tuliokuwa tunahitaji kutekeleza mradi huu, na tulitegemea mradi kwa sasa ufikie asilimia 31 lakini katika hali ya kushangaza mradi umefikia asilimia 24 tu jambo ambalo halikubaliki.” amesema Dk. Biteko.

Ameeleza kuwa, sababu zilizotolewa na mkandarasi za kuchelewesha mradi miongoni mwao ni wananchi kugoma kutoa maeneo kwa madai ya fidia.

Ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutumia mapato yake ya ndani kulipa fidia wananchi waliopisha mradi.

Dk. Biteko ameeleza kuwa mkandarasi alishaagizwa asiutekeleze mradi huo kwa mazoea kutokana na umuhimu wake kwani kwa sasa miundombinu inayosafirisha umeme kwenda Dodoma kutoka mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) kupitia kituo cha Chalinze inabeba umeme kidogo kwa takriban megawati 240 tu ambayo ni sawa na mashine moja tu kati ya mashine tisa za JNHPP, hivyo njia hiyo mpya ya umeme ya kV 400 inayojengwa ni muhimu.

spot_img

Latest articles

Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa wito wa utawala bora kuimarisha uwekezaji wa umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio...

TTB yamkaribisha bingwa wa Masumbwi duniani Terence kwa ziara ya utalii

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini...

DAWASA yasisitiza matumizi ya bidhaa za ndani kuimarisha huduma ya maji

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

More like this