Na Mwandishi Wetu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka viongozi wa klabu ya Yanga, kutathmini uhalali wao wa kuongoza klabu hiyo kwa kitendo cha kukichangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) sh 100 milioni.
Taarifa ya Chadema iliyotolewa leo tarehe 15 Agosti 2025, na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, Brenda Rupia.
Katika taarifa hiyo Rupia ameeleza kuwa kitendo cha Yanga kuichangia CCM ni dharau kwa wanachama na mashabiki wenye itikadi za vyama mbalimbali za siasa.
Rupia ameeleza kuwa taarifa ya yanga ya kudai kuwa mchango huo ulitoka kwa GSM haikuwa ya kweli kwa kuwa taarifa za awali zilidai kuwa GSM, amechangia sh.10 Bilioni, huku Yanga ikichangia sh.100 milioni.
Katika hatua nyingine Yanga imeondoa katika mitandao yake ya kijamii taarifa ya ufafanuzi waliyoandika kwa Umma jana juu ya mchango huo, pamoja na kuwaomba radhi mashabiki waliyoitoa jana Agosti 14,2025.