Elimu ya Nishati Safi ya kupikia yawafikia wanawake mkoani Mbeya

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imetoa wito kwa wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia na kutumia nishati safi ya kupikia kama vile umeme na gesi ikiwa ni njia pia ya kulinda afya, mazingira na kuimarisha uchumi wa kaya.

Wito huo umetolewa leo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Deo Alex katika Kongamano la Wanawake na Wajasiriamali kuhusu fursa za kiuchumi lililofanyika mkoani Mbeya.

Amesema kuwa mwaka 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa maelekezo ya kuandaliwa kwa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mwanzo wa safari ya kuelekea katika matumizi ya nishati iliyosafi ya kupikia.

Ameeleza kuwa kufuatia agizo hilo, Wizara ya Nishati iliandaa mkakati huo na kuuzindua rasmi mwaka 2024 ambapo utekelezaji wake umeanza rasmi.

Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa mkakati huo, matumizi ya nishati isiyo safi yameonekana kuwa chanzo kikuu cha athari mbalimbali, ikiwemo uharibifu wa mazingira na matatizo ya kiafya kwa watumiaji, miongoni mwa athari za kiafya zilizobainishwa ni pamoja na saratani, homa za mapafu, ujauzito kuharibika na kujifungua watoto kabla ya muda.

Ameeleza kuwa gharama za kumtibu mtu mwenye saratani ni kubwa ukilinganisha na gharama ya ununuzi wa nishati safi ya kupikia kama vile mtungi wa gesi, hivyo wananchi wanahimizwa kuwekeza katika matumizi ya nishati salama kwa ajili ya afya zao na mazingira.

Alex amebainisha kuwa mkakati huo umefungua fursa mbalimbali kwa wajasiriamali, ikiwa ni pamoja na kuwa mawakala wa gesi na nishati nyingine mbadala.

Amezitaja aina za nishati safi zinazopendekezwa kuwa ni pamoja na umeme, gesi na mkaa mbadala.

Wanawake mbalimbali waliohudhuria Kongamano hilo kwa nyakati tofauti wameishukuru Wizara ya Nishati kwa kuwapa elimu hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia na kutoa wito kuwa iendelee hadi ngazi ya vijiji.

Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, likiwa na kauli mbiu isemayo “Changamkia Fursa, Jenga Leo na Kesho Yako.”

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...