Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Dodoma Jiji yamtangaza kocha Vincent Mashami kutoka Polisi FC ya Rwanda akichukua nafasi ya Mecky Maxime aliyeondoka mwishoni msimu uliomalizika.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo leo Agosti 6, 2025, Mashami amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Katika hatua nyingine Dodoma Jiji imemtambulisha kiungo, Nelson Munganga raia wa DR Congo akitokea Tabora United.
Munganga mwenye umri wa miaka 32 aliwahi kuitumikia klabu ya AS Vita na DC Motema Pembe ya Cobgo DRC na Moulodia, MAS Fes za Morocco.
Dodoma Jiji inaimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya msimu uliopita kumaliza katika nafasi 12 na pointi 34.