Januari Makamba hayumo, Nape apeta uteuzi CCM

Na Mwandishi wetu

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla amejata majina ya wagombea sita wa  Jimbo Bumbuli mkoani Tanga  ambapo  aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kipindi kilichopita  Januari Makamba jina lake halijapita.

Makalla ametaja orodha ya majina ya wateule wa jimbo hilo watakaokwenda kupigiwa kura za maoni leo Julai 29,2025, jijini Dodoma, ambao ni Hidaya Kilima, Zahoro Rashid Hanuna, Eng. Ramadhan Singano, Rashid Salimu, Silas Joram na John Aloyce.

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye atachuana na wagombea watatu ambao ni Jemedari Said, Jabiri Chilumba na Metta Nahonyo katika kulitetea Jimbo

Aidha aliyekuwa kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko, amepenya katika katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, Jimbo la Tarime Mjini mkoani Mara akiwa miongoni mwa wagombea sita walioteuliwa.

spot_img

Latest articles

Kwa nini ninatamani Polepole anyamaze milele?

JUMATATU wiki hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipitisha majina ya wanachama wake watakaopigiwa kura...

Mnyama Simba anaachia tu vifaa vyake

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba leo Julai 30, 2025, imemtambulisha Alassane Kante raia wa...

Chalamila awaalika wakazi wa Dar kujitokeza kwa wingi uzinduzi wa Kituo cha biashara cha EACLC

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaalika Watanzania na...

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

More like this