‘Dar Boxing Derby’ unaambiwa ulingo utatitia Leders Club kesho

Na Winfrida Mtoi

Hatimaye ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wadau, wapenzi wa ngumi imefika ambapo kesho yatapigwa mapambano ya ngumi za kulipwa ‘Dar Boxing Derby’ yakihusisha mabondia wenye upinzani mkali kutoka pande tofauti za mitaa ya Dar es Salaam.

Katika mapambano hayo zaidi ya 10, moja pekee litahusisha bondia kutoka nje ya nchi ambapo Mfaume Mfaume atapigana  dhidi ya Mmalawi, Kudakwache Banda.

 Pambano ambalo limevuta zaidi hisia za mashabiki wa mchezo huo ni lile linalowakutanisha wachezaji wa Yanga, Kibwana Shomari na Denis Nkane ambao pamoja na kucheza soka wamejitosa katika masumbwi.

 Wachezaji hao wamejumuika na mabondia wengine leo Julai 25, 2025, katika zoezi la kupima uzito katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Dar es Salaam ambako mapambano hayo yatapigwa.

 Katika zoezi hilo la kupima uzito lilifanyika, Kibwana amepata kilo 60.5 na Nkane 61, hivyo kutangazwa kucheza uzito mwepesi (lightweight).

 Mapambano mengine yanayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Ibrahim Class dhidi ya Nassib Ramadhani, Karim Mandonga na Shaban Kaoneka kutokana na kuwa na kisasi.

 Mandoga anataka kulipa kisasi kwa Kaoneka ambaye alimpiga katika pambano la mwisho walilokutana kama ilivyo kwa Nassib aliyepania kulipa kisasi kwa Class.

 Kwa upande wa Mfaume Mfaume anatumia fursa hiyo kuwaonesha mashabiki wake kuwa bado yupo fiti baada ya kutoonekana ulingoni kwa muda mrefu.

Wanawake pia hawakuacha nyuma ambapo Debora Mwenda atachapana na Asia Meshack, huku Sarah Alex akipigana na Stumai Muki.

 Akizungumzia maandalizi wa mapambano hayo, Meja Selemani Semunyu, amesema maandalizi yote ya mekamilika na burudani itaanza mapema na milango itakuwa wazi kuanzia saa 6:00 mchana.

 Amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi bila kuhofia chochote kutokana na kuwepo kwa ulinzi wa kutosha pamoja na sehemu ya kukaa watazamaji kupangwa kwa utaratibu ambao kila mmoja atakaa kwa utulivu kushuhudia burudani.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this